Sunday, May 25, 2014
VIKAO BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUANZA KESHO
Do you like this story?
Bunge
la Afrika Mashariki (Eala), linaanza vikao vyake kesho. Bunge hilo lilivunjika
Aprili Mosi mwaka huu kutokana na vurugu zilizosababishwa na hoja ya kumng’oa
Spika Margrethe Zziwa.
Pamoja
na mambo mengine, vikao vya Bunge hilo vinavyoanza kwa wabunge kukutana kwenye
kamati mbalimbali, litajadili na kupitisha bajeti ya mwaka wa fedha ya
2014/2015.
Mkuu
wa Idara ya Mawasiliano ya Sekretarieti ya EAC, Richard Othieno-Owora alisema
jana kuwa Spika Zziwa, ambaye tayari wabunge 37 wametoa hoja ya kutokuwa na
imani naye ndiye atakayeongoza vikao.
Mwenyekiti
wa Baraza la Mawaziri wa EAC, Phyllis Kandie, ndiye atakayewasilisha Bajeti ya
EAC inayotarajiwa kuongezeka kutoka Dola milioni 131.8 bilioni za mwaka jana.
Miongoni
mwa miradi na maeneo inayotengewa fedha kwenye bajeti ya EAC ni kilimo,
biashara, ulinzi na usalama, miundombinu na elimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VIKAO BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI KUANZA KESHO”
Post a Comment