Friday, May 9, 2014
LICHA YA SKENDO KIBAO ZINAZOMUANDAMA, CHAMA CHA ANC CHA RAIS JACOB ZUMA KINAONGOZA.
Do you like this story?
Wakuu wa tume ya uchaguzi nchini
Afrika-Kusini wametangaza kuwa shughuli ya kuhesabu kura inaenelekea kukamilika
baada ya uchaguzi mkuu uliofanyika juzi kwa mara ya tano tangu utawala wa
mwafrika mzungu.
Chama tawala cha ANC kinaongoza kwa
zaidi ya asilimia 63, huku kile cha Democratic Alliance kikiwa na asilimia 23.
Chama kipya cha Economic Freedom
Fighters cha Julius Malema kikiwa katika nafasi ya tatu.
Jumla ya asilimia 96 ya kura
zilizopigwa zimehesabiwa.
Mwandishi wa BBC Andrew Harding anasema
kuwa ukosefu wa ajira,ufisadi na ukosefu wa usawa katika jamii ni changamoto
kubwa lakini wapiga kura bado wana imani na chama cha ANC.
Tume ya uchaguzi imesema kuwa uchaguzi
ulifanyika kwa amani katika maeneo mengi ya nchi huku asilimia 73 ya wapiga
kura wakijitokeza kupiga kura.
Uchaguzi huu ni wa kwanza tangu nchi
hiyo kuondokewa na rais wa kwanza mzalendo wa nchi hiyo hayati Nelson Mandela.
Afrika Kusini imetimiza miaka 20 tangu kumalizika kwa utawala wa wazungu.
Idadi kubwa ya wananchi imekuwa
ikilalamikia utenda kazi wa serikali hasa kwa kuwa kuna kiwango kikubwa cha
ukosefu wa ajira.
Wadadisi wanasema kuwa chama cha ANC
huenda kikatumia fursa hii kuimarisha uchumi wa nchi hasa baada ya miaka mitano
ya kile kinachosemekana kuwa utawala mbovu wa Rais Jacob Zuma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ LICHA YA SKENDO KIBAO ZINAZOMUANDAMA, CHAMA CHA ANC CHA RAIS JACOB ZUMA KINAONGOZA.”
Post a Comment