Friday, May 9, 2014
KAFULILA AWALIPUA MAWAZIRI AKAUNTI YA ESCROW.
Do you like this story?
Mbunge
wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila jana aliibua tuhuma nzito
bungeni akiwahusisha mawaziri wawili na Sh200 bilioni zilichotwa katika Akaunti
ya Escrow, iliyokuwa inamilikiwa kwa pamoja kati ya Tanesco na Kampuni ya kufua
umeme ya IPTL.
Katika
tuhuma hizo, alimuunganisha pia Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini na vigogo wengine, wakiwamo wa Benki Kuu ya
Tanzania (BoT) na wa Serikali, wote akiwataja tu kwa vyeo bila majina.
Mawaziri
waliotajwa ni Waziri wa Nishati na Madini, Waziri wa Fedha na Mkurugenzi wa
Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco).
Ingawa
Kafulila hakutaja kwa majina, Waziri wa Nishati ni Profesa Sospeter Muhongo, wa
Fedha ni Saada Mkuya, Katibu Mkuu wa wizara hiyo (Nishati) ni Eliakim Maswi na
AG ni Frederick Werema.
Kafulila
alitoa tuhuma hizo bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya Makadirio ya Mapato
na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa Mwaka wa Fedha 2014/15.
Mbunge
huyo alisema fedha zilizoibwa katika Akaunti ya Escrow ni nyingi kuliko zile
zilizoibwa katika kashfa ya Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ya BoT mwaka 2005.
“Pamoja
na hilo, Watanzania wamekuwa wakisikia kwenye vyombo vya habari kwamba Tanesco
wakati ilipokuwa na mgogoro na IPTL walifika mahali wakafungua akaunti ya
Escrow,” alisema.
Mbunge
huyo alisema akaunti hiyo ilifunguliwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), mwaka 2004
na hadi jana, akaunti ile ilishafikia Dola za Marekani 122 milioni,” alisema
Kafulila.
Alisema
fedha hizo ziliwekwa kwa lengo maalumu kutokana na mgogoro uliokuwapo kati ya
IPTL na Tanesco ili ziweze kusaidia malipo baada ya mgogoro kuisha katika
Baraza la Usuluhishi wa Kibiashara la ISCID.
Alitaka
jambo hilo liingie kwenye rekodi kwa kuwa linahusu BoT na vigogo akiwamo
Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Waziri wa Nishati na Madini pamoja na Katibu wake
na pia Waziri wa Fedha.
Alisema
wakati Tanesco ikidaiwa madeni zaidi ya Sh400 bilioni, viongozi hao
wameidhinisha kugawanywa kwa fedha hizo kihuni jambo alilosema halivumiliki
hata kidogo.
Kafulila
alisema fedha hizo zilichotwa na Kampuni ya PAP aliyosema ya “Singasinga na ya
kitapeli” ambayo iliidhinishiwa kuchota fedha hizo kinyume na utaratibu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KAFULILA AWALIPUA MAWAZIRI AKAUNTI YA ESCROW.”
Post a Comment