Monday, May 5, 2014
MASHABIKI WA SOKA MBEYA WAPEWA `TANO` NA MREFA, VIONGOZI WASEMA MAMBO MAZURI YAJA.
Do you like this story?
CHAMA cha soka mkoani Mbeya, MREFA
kimewashukuru mashabiki wa soka ndani na nje ya mkoa huo kwa kujitokeza
kuishangilia timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa stars dhidi ya Malawi.
Mechi hiyo iliyomalizika kwa suluhu
pacha ya bila kufungana, Stars ikiingozwa kwa mara ya kwanza na kocha mpya,
Mart Nooij ilichezwa kwenye uwanja wa sokoine jijini Mbeya.
Akizungumza na mtandao huu jioni hii,
katibu mkuu wa MREFA, Seleman Haroub amesema mechi ilimalizika salama na kwa
asilimia kubwa walipata mafanikio.
“Tunashukuru mechi imefanyika salama na
kila kitu kimekwenda sawa. Mashabiki walijitahidi kujitokeza na nadhani inatupa
taswira kuwa siku za usoni TFF watatufikiria zaidi”.
“TFF wameonesha kutujali sana na
kutuletea mechi ya timu ya taifa kwa mara ya kwanza, hakika tunayafanyia kazi
mapungufu yaliyopo katika uwanja wetu ili tupewe mechi nyingi zaidi”. Alisema
Haroub.
Aidha, amesema ukarabati wa uwanja bado
unaendelea hasa kujenga vyoo vya kisasa kwa lengo la kuufanya uwe na hadhi kubwa ya kimataifa.
Katika mechi ya jana, Kocha Nooij
aliamua kuwatumia wachezaji wenye uzoefu na michuano ya ligi kuu soka Tanzania
bara badala ya wale waliopatikana katika mpango wa maboresho ya timu hiyo.
Kitendo cha kocha Nooij kuwaacha
wachezaji waliochagulia kutoka katika mpango wa maboresho kimezua hisia tofauti
kwa wadau wa soka.
Wengi wamekuwa wakisikika kuwa
wachezaji hao hawana kiwango cha kuichezea Taifa stars na kuifikisha fainali ya
kombe la mataifa ya Afrika, AFCON mwakani nchini Morocco.
Lakini baadhi ya wadau wanasisitiza
wachezaji hao wapewe muda na kuaminiwa ili kuiletea mafanikio Taifa stars.
Mechi ya jana ilikuwa ya pili kwa Taifa
stars ya maboresho ambapo aprili 26 mwaka huu siku ya maadhimisho ya miaka 50
ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ilicheza dhidi ya Burundi na kulala mabao
3-0.
Mechi dhidi ya Burundi, kaimu kocha kwa
wakati ule, Salum Madadi aliwatumia zaidi wachezaji wa kikosi cha maboresho,
lakini jana bosi wake, Nooij akawatoa kabisa katika mpango wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MASHABIKI WA SOKA MBEYA WAPEWA `TANO` NA MREFA, VIONGOZI WASEMA MAMBO MAZURI YAJA.”
Post a Comment