Monday, May 12, 2014
MBARONI KWA KUUA WAZAZI WAKE WAWILI KIKATILI”KILIMANJARO.
Do you like this story?
. |
Baadhi ya waombolezaji wakiwa katika kijiji cha Roo, Tarafa ya Masama, Wilaya ya Hai mkoani Kilimanjaro, wakiwa katika sala ya mazishi ya marehemu iliyofanyika Mei 10, 2014, ambapo Shahidu Njau na mkewe Minei Swai, walipokutwa na mauti baada ya kucharangwa/katwa mapanga na mtoto wao. |
JESHI la
Polisi mkoani Kilimanjaro, linamshikilia Yusufu Njau (32), mkazi wa kijiji cha
Roo Wilayani Hai mkoani humo, kwa kosa la kuwauwa wazazi wake ‘kikatili’ kwa
kuwakata na mapanga kichwani na kisha kuchoma moto nyumba waliyokuwa wanaishi
wazazi hao.
Kamanda wa
Polisi mkoani humo, Robert Boaz, ameiambia FikraPevu
Jumatatu Mei 12, 2014 kuwa mtuhumiwa huyo aliyefanya
kitendo cha kinyama Mei 09, 2014 saa kumi na mbili za jioni nyumbani kwao,
ambapo kupitia msako ulioendeshwa na Jeshi hilo kuanzia siku ya tukio ambapo
leo (Jumatatu) saa mbili asubuhi lilimkamata akiwa nyumbani kwa kaka
yake Alifa Shaibu.
Boaz,
amesema mtuhumiwa alimuua Baba yake mzazi, Shahibu Hassan (60), pamoja na Mama
yake mzazi, Minae Mohamed (57), ambao waliozikwa Jumamosi, Mei 10 2014 katika
Naye
Mwenyekiti wa kijiji cha Roo, Alfani Swai, alisema mtuhumiwa huyo alitoka
kutoka alipokuwa amejificha baada ya kukumbwa na njaa kali ndipo alipoenda
nyumbani kwa kaka yake ‘Alifa Shaibu’ kwa nia ya kuomba chai.
Amesema
mara baada ya mtuhumiwa huyo kufika kwa Kaka yake alipata simu kuwa mtuhumiwa
huyo yuko katika nyumba hiyo, ndipo alipowasili na kumpeleka mtuhumiwa katika
katika kituo cha Polisi Bomang’ombe.
Mara baada
ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo wananchi wa kijiji hicho walisema kwa sasa
wataishi kwa amani kijiji hapo, kutokana na kuwa na mashaka na mtuhumiwa huyo
aliyekuwa akisumbua kijiji hicho kwa muda mrefu.
Kumbukumbu
zinaonyesha kuwa hali ya usalama nchini, inaonekana kutia shaka wananchi
kufuatia mfululizo wa matukio ya watu kutekwa, kuteswa hata kuuawa kwa ndugu wa
familia moja wa watoto na baada ya mda watuhumiwa huripotiwa kukamatwa katika
maeneo mbalimbali nchini na sheria kuelezwa inaanza kuchukua mkondo wake kwa
kuanzisha upelelezi wa matukio hayo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBARONI KWA KUUA WAZAZI WAKE WAWILI KIKATILI”KILIMANJARO.”
Post a Comment