Monday, May 12, 2014
TAIFA STARS YA MART NOOIJ KUUMANA NA ZIMBABWE DAR JUMAPILI.
Do you like this story?
Mechi ya kwanza
ya raundi ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza Fainali za Afrika 2015 nchini
Morocco kati ya Tanzania (Taifa Stars) na Zimbabwe (Mighty Warriors) itafanyika
Jumapili (Mei 18 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Awali mechi
hiyo tulipanga ichezwe Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya kwa nia ya kuhakikisha
mikoa yote ya Tanzania inapata fursa ya kuwa mwenyeji wa mechi za kimataifa.
Ili Uwanja wa
Sokoine uweze kuchezwa mechi za kimataifa za mashindano, Shirikisho la Mpira wa
Miguu Afrika (CAF) lilituma Mkaguzi (inspector) wake kwenye uwanja huo Jumamosi
(Mei 10 mwaka huu) ambapo imeamua kuwa marekebisho yanayofanyika hayatamalizika
katika muda stahili, hivyo mchezo huo kutochezwa Sokoine.
Tunatoa mwito
kwa wamiliki wote wa viwanja kuwasiliana na TFF ili Idara ya Ufundi iwaelekeze
maboresho ya kufanya ili viwanja vingi iwezekanavyo viweze kukidhi viwango
vinavyotakiwa na CAF na Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA).
Taifa Stars
ambayo ilikuwa kambini mkoani Mbeya itarejea Dar es Salaam keshokutwa (Mei 14
mwaka huu) kujiandaa kwa mechi hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAIFA STARS YA MART NOOIJ KUUMANA NA ZIMBABWE DAR JUMAPILI.”
Post a Comment