Sunday, May 11, 2014
MBEYA CITY NDANI YA MTO NILE.
Do you like this story?
Timu
ya Mbeya City imeteuliwa kushiriki mashindano ya Shirikisho la Baraza la Vyama
Vya Soka Afrika Mashariki na Kati (Cecafa) yajulikanayo kama Kombe la Mto Nile
(Cecafa Nile Basin) yatakayofanyika nchini Sudan kuanzia Mei 22 hadi Juni 4
mwaka huu.
Katibu
Mkuu wa Cecafa, Nicholas Musonye alitangaza uteuzi huo kwa waandishi wa habari
jijini Mbeya mara baada ya kufanya kazi ya kukagua Uwanja wa Sokoine kama
unafaa kuchezewa mechi za kimataifa, akiwa ameambatana na Mkurugenzi wa Ufundi
wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Salum Madadi.
Kwa
mujibu wa Katibu Mkuu huyo, mashindano hayo mapya hushirikisha timu zilizoshika
nafasi ya pili katika ligi za nchi wanachama, ambapo kwa Tanzania, Yanga ndiyo
ilitakiwa kushiriki michuano hiyo, lakini walisema hawapo tayari kushiriki.
Alisema
kuwa hata walipoiteua timu ya Azam ambayo ndiyo mabingwa wa Ligi ya Tanzania
Bara waligoma kushiriki wakidai kuwa wachezaji wao wapo likizo.
Alisema
kuwa Cecafa kwa kushirikiana na TFF waliona ni vyema kuiteua Mbeya City ambayo
imeshika nafasi ya tatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MBEYA CITY NDANI YA MTO NILE.”
Post a Comment