Saturday, May 17, 2014

MSANII WALTER CHILAMBO APATA AJALI YA GARI.






Ajali imetokea saa sita kasoro usiku May 15 2014 Kimara Dar es salaam ambapo mwimbaji Walter ambae ni mshindi wa BSS 2013 akiwa barabarani anaendesha alipata mshtuko mkubwa baada ya gari iliyokua nyuma yake kuja kwa kasi na kumchomekea kwa mbele na kumsukuma.

Kwa mlio uliotokea na jinsi tukio lenyewe lilivyokuwa Walter alipata mshtuko na kupanic kwa muda kabla ya kuanza kurejea kwenye hali yake kutokana na ajali hii ambayo haikumpa jeraha lolote.

Kwa jinsi jamaa wa gari jingine alivyomvamia unaweza kuhisi labda alikua anayo nia ya kumuumiza Walter au alipania kumgonga isivyo kawaida manake toka alipokuwa nyuma ya Walter alikua akimuwashia taa kwa mwanga mkubwa kuashiria anataka kupita.

Baada ya kumwashia Walter taa kwa muda mrefu ilipopatikana nafasi ya kumpisha alimwachia ila kabla hajapita huyu jamaa aliekua na wenzake wanne walifungua vioo na kuanza kumtukana Walter kisha akamchomekea mbele kwa makusudi ndio Walter akagonga mbele kisha ukuta wa barabara na bampa likaingia chini ya matairi na jamaa wale wakakimbia bila Walter kuweza kushika hata namba za gari.

Walter anasema ‘wale jamaa ilikua kama wanakimbizwa huko walikotoka’Uwapo barabarani Dar es salaam unashauriwa kumpisha yeyote anaetaka kupita kama kuna nafasi, Mwaka jana kuna dereva wa daladala aliuwawa kwa risasi na watu waliokua kwenye pikipiki waliotaka awapishe lakini akawa anawanyima nafasi ambapo walipopata upenyo wa kumpita eneo la Sinza Kumekucha jamaa aliekua kapakiswa kwenye pikipiki alifyatua risasi iliyomuua palepale dereva wa daladala.

Kabla ya kumuua yalitokea majibizano kidogo ambapo iliripotiwa Dereva wa daladala kama kawaida yao akajibizana nao na kuwauliza watamfanya nini, wasepe zao waache kumbabaisha.

0 Responses to “MSANII WALTER CHILAMBO APATA AJALI YA GARI.”

Post a Comment

More to Read