Saturday, May 17, 2014

WANANCHI WA IRINGA WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA VIRUSI VYA UKIMWI.





Mratibu wa kuthibiti ukimwi halmashauri ya manispaa ya iringa sekta ya  afya BONAVENTURA KALUMBETE amewataka wananchi wa  manispaa ya iringa kuendelea kujitokeza kwa wingi katika upimaji wa virusi vya ukimwi , magojwa ya zinaa, na katika huduma ya tohara.

KALUMBETE amesema kuwa ameridhishwa na mwitikio  wanao uonyesha kwa kujitokeza kwa wingi katika upimaji wa magonjwa hayo.

Mratibu huyo ameongeza kuwa waliojitokeza kupima virusi vya ukimwi mwezi uliopita jana ni  2,541,na waliojitokeza kupima magonjwa ya zinaa ni 306 wakati waliojitokeza kupata huduma ya tohara ni 356 hali inayoonesha kuwa elimu juu ya uthibiti wa magojwa ambukizi imeenea mkoani hapa.

KALUMBETE amesema mkoa wa iringa umefanikiwa kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka nafasi ya kwanza kitaifa kwa  asilimia 15.7 mwaka 2007/2008 hadi kufikia nafasi ya pili kwa sasa ikiwa na asilimia 9.1 wakati nafasi ya kwanza ikishikiliwa na mkoa wa njombe kwa asilimia 14.8.

Aidha amewataka vijana kuwa na tabia ya  kupima afya  kabla ya kuanza mahusiano .

0 Responses to “WANANCHI WA IRINGA WATAKIWA KUJITOKEZA KWA WINGI KUPIMA VIRUSI VYA UKIMWI.”

Post a Comment

More to Read