Saturday, May 17, 2014

CHELSEA? MAN UNITED? AU BAYERN MUNICH? SOMA NI KLABU GANI YA ULAYA INAYOONGOZA KWA WACHEZAJI WAKE WENGI KWENDA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014



Bado ana nguvu: Kiungo wa Chelsea, Frank Lampard (kulia) ametajwa katika kikosi cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya England
Ardhi ya nyumbani: Beki wa Brazil ,  David Luiz ni miongoni mwa wachezaji  18 wa Chelsea wanaotarajia kushiriki kombe la dunia mwaka huu na nchi zao.


KLABU ya Chelsea ndio timu pekee ambayo wachezaji wake wengi wanaenda kushiriki fainal za kombe la dunia kuanzi mwezi ujao nchini Brazil.

Wachezaji 18 wa Chelsea wanatarajia kuzichezea nchi zao katika fainali hizo kubwa za soka duniani.

Ukiangalia vikosi vya awali vya mataifa mbalimbali na vikosi vya mwisho vya watu 23 , wachezaji wengi wa Chelsea wamechaguliwa, huku wakifuatiwa na Manchester United ambayo wachezaji wake 16 wamechaguliwa licha ya kuwa na msimu mbovu.

Kwa wenyeji Brazil, kocha Luiz Felipe Scolari amewaita Oscar, Willian, Ramires na  David Luiz kuichezea nchi yao katika ardhi ya nyumbani.

KLABU AMBAZO WACHEZAJI WAKE WENGIN WANAKWENDA KOMBE LA DUNIA

1. Chelsea (18)
2. Manchester United, Bayern Munich (16)
3. Napoli (14)
4. Barcelona, Real Madrid, Manchester City (13)
5. Juventus, Arsenal, Liverpool (12)
6. Atletico Madrid (11)
7. Porto, Inter Milan, AC Milan, Zenit (10)
8. Borussia Dortmund, Paris Saint-Germain (8)
9. Southampton, Schalke, Roma (7)

0 Responses to “CHELSEA? MAN UNITED? AU BAYERN MUNICH? SOMA NI KLABU GANI YA ULAYA INAYOONGOZA KWA WACHEZAJI WAKE WENGI KWENDA KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014”

Post a Comment

More to Read