Friday, May 30, 2014
MTANZANIA JERA MIAKA 3 KWA UCHAWI."KENYA"
Do you like this story?
Mchawi
kutoka Tanzania amehukumiwa kifungo cha miaka mitatu nchini Kenya kwa kumlaghai
mwanamke mfanyabiashara mkenya na kumuibia shilingi milioni tisa.
Mchawi
huyo alimhadaa mama huyo kuwa kwa kupitia njia za kichawi angeweza kuzifanya
pesa hizo kuwa maradufu yaani milioni 18.
Bwana
Amos Chipeta pia ataongezwa kifungo cha miezi tatu kwa kupatikana na vifaa
vinavyoumiwa kufanya uchawi kama vile chupa, visu na ngozi ya Paka.
Kwa
mujibu wa mtandao wa Daily Nation, Chipeta alihukumiwa pamoja na mwenzake bwana
Peter Christopher aliyepatikana na hirizi zinazotumika kufanyia uchawi.
Bwana
Chipeta alimlaghai Bi Catherine Njeri hela zake tarehe tofauti tofauti kati ya
mwezi wa Agosti na Decemba 2012 baada ya mwanamke huyo kuwaendea na kumwomba
wazifanye pesa hizo ziwe maradufu
Walijitetea
kwa kusema kuwa mwanamke huyo aliwaendea ili wampe nguvu za kichawi aweze
kuwashinda wapinzani wake wa kisiasa
Maafisa
wa polisi walipata hirizi hizo na vifaa walivyotumia kwa uchawi mwezi Februari
1, 2014 katika nyumba ya kukodisha iliyo kando ya barabara ya Juja viungani mwa
mji mkuu Nairobi.
Hakimu
aliyesikiliza kesi hiyo alisema kuwa wanaume hao waliona mwanamke huyo kuwa
mjinga na basi kumnafiki kwa urahisi na kuwa hawana majuto au toba.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTANZANIA JERA MIAKA 3 KWA UCHAWI."KENYA"”
Post a Comment