Saturday, May 31, 2014

PIGO TENA BONGO MUVI: GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA.




NI pigo tena kwa tasnia ya Bongo Muvi, mwongozi filamu Bongo na aliyekuwa mume wa staa wa filamu za Kibongo, Yvonny Cherry 'Monalisa', George Tyson amefariki dunia baada ya kupata ajali mbaya ya gari maeneo ya Gairo, Morogoro akitokea mkoani Dodoma.

Tyson alikuwa ameambatana na watu kadhaa katika safari hiyo ambao wanadaiwa kuumia vibaya. Mwili wa marehemu Tyson pamoja na majeruhi wa ajali hiyo wamepelekwa Hospitali ya Mkoa wa Morogoro. Tyson enzi za penzi lake na Monalisa walifanikiwa kupata mtoto aitwaye Sonia.

0 Responses to “PIGO TENA BONGO MUVI: GEORGE TYSON AFARIKI DUNIA.”

Post a Comment

More to Read