Friday, May 30, 2014
MUSWADA WA VAT WAONGEZA MUDA WA BUNGE.
Do you like this story?
Spika
wa Bunge, Anne Makinda amesema muda wa Bunge utaongezwa ili kutoa nafasi kwa
serikali kuwasilisha Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Kodi ya Mapato (VAT).
Wiki
iliyopita, Mbunge wa Mwibara, Kangi Lugola aliomba mwongozo na alipopewa nafasi
alimlalamikia Spika wa Bunge kuwa katika ratiba ya bunge, haoni mahali ambapo
kuna nafasi ya wabunge kujadili Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya VAT.
Lugola,
(CCM) baada ya kauli yake, alitishia kukusanya saini za wabunge kumwondoa Spika
Makinda iwapo muswada huo hautaletwa katika Bunge la Bajeti na zaidi ni kwa
ajili ya kufuta misamaha ya kodi isiyo na tija
.
Muda
mfupi baada ya kupitishwa kwa bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi kwa mwaka wa fedha 2014/2015, Makinda alitangaza hatua hiyo ya Bunge
kuongeza muda.
“Kwa
mujibu wa kanuni zetu hatuingizi kitu kingine katika Bunge la Bajeti zaidi ya
bajeti, lakini tunaangalia uwezekano wa kuongeza muda baada ya bajeti kwa siku
chache kwa sababu ya mambo yanayotakiwa kufanyika,” alisema na kuongeza;
“Naambiwa
kuwa Serikali inataka kuleta sheria inayohusiana na VAT.”
Makinda
aliwataka wabunge kusoma vizuri kanuni za Bunge kwa sababu Spika hahusiki
kuletwa muswada bungeni.
Katika
hoja yake, mbunge huyo wa Mwibara, alisema nchi inapoteza Sh1.5 trilioni kwa
misamaha ya kodi wakati bajeti ya Serikali kwa mwaka jana ina upungufu wa kiasi
hicho hicho cha fedha.
Makinda
alisema kuwa kuongezwa kwa siku hizo kunalenga kuwawezesha wabunge kujadili
ripoti ya migogoro ya ardhi nchini.
Alisema
Kamati ya Bunge iliyopewa kuchunguza migogoro hiyo ilikwenda mbali zaidi na
kuona vitu vingi ikiwemo matatizo yaliyopo katika mfumo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MUSWADA WA VAT WAONGEZA MUDA WA BUNGE.”
Post a Comment