Friday, May 30, 2014
JAJI WA PILI ABWAGA MANYANGA KESI YA JENGO LILILOUA DAR GHANDI
Do you like this story?
Hili ndio gorofa lililoanguka dar |
Washtakiwa |
. Jaji Raziah Sheikh aliyekuwa amepangwa kusikiliza maombi ya
washtakiwa wa kesi ya mauaji ya jengo lililoporomoka katika Mtaa wa Indira
Gandhi, amebwaga manyanga kuendelea kuisikiliza kesi hiyo.
Katika
maombi hayo, washtakiwa hao wanaiomba mahakama kuu ipitie uamuzi wa Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu wa kuwanyima dhamana bila kupewa haki ya kusikilizwa ili
kujiridhisha na usahihi na uhalali wa uamuzi huo uliotolewa Machi 12, 2014.
Pia
wanaiomba mahakama hiyo itafakari na kupitia hati ya mashtaka waliyofunguliwa
na mjibu maombi (Jamhuri), ya kubadilishiwa mashtaka kutoka mashtaka ya kuua
bila kukusudia na kuwa ya kuua kwa kukusudia, ambayo ilikubaliwa na Mahakama ya
Kisutu, wanayodai ni kinyume cha sheria.
Maombi
mengine ni Mahakama Kuu ipitie amri zilizotolewa na Mahakama ya Kisutu kukubali
mashtaka mapya bila mjibu maombi kuijulisha Mahakama mazingira yaliyosababisha
kuibuka kwa mashtaka hayo mapya au kuwapa waombaji (washtakiwa) nafasi ya
kusikilizwa kwa mujibu wa sheria.
Washtakiwa
hao pia wanaiomba Mahakama Kuu kupitia amri ya Mahakama ya Kisutu kuwafutia
dhamana bila haki ya kusikilizwa, na pia wanaiomba Mahakama itupilie mbali hati
ya mashtaka mapya ya kuua kwa makusudi badala ya kuua bila kukusudia.
Maombi
hayo yalitarajiwa kuanza kusikilizwa jana, lakini Jaji Sheikh alitangaza
kujitoa katika usikilizwaji wa maombi hayo .
Badala
yake aliamuru jalada la kesi hiyo lirejeshwe kwa Jaji Mfawidhi ili lipangiwe
jaji mwingine wa kusikiliza maombi hayo na kupanga shauri hilo litajwe Juni 2,
2014, mahakamani hapo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “JAJI WA PILI ABWAGA MANYANGA KESI YA JENGO LILILOUA DAR GHANDI”
Post a Comment