Friday, May 30, 2014
SUMATRA YAFUNGA KITUO CHA DALADALA MWENGE.
Do you like this story?
Mamlaka
ya Udhibiti wa Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (Sumatra) imetangaza kuhamisha
kituo maarufu cha daladala cha Mwenge kwenda eneo la Makumbusho.
Katika
taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, ofisa mfawidhi wa Sumatra wa Kanda ya
Mashariki, Conrad Shio alisema Kituo cha Mwenge kitafungwa rasmi Jumapili na
eneo hilo litabaki wazi kupisha upanuzi wa Barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Shio
alieleza sababu ya kuhamisha kituo hicho kuwa ni ufinyu wa eneo lenyewe jambo
linalosababisha magari kushindwa kuingia kituoni hapo kwa wakati, hasa nyakati
za asubuhi na jioni. Hali hiyo husababisha foleni kubwa isiyo ya lazima.
Alisisitiza
madereva wote kutii agizo hilo kuanzia Jumatatu na kwamba atakayekiuka agizo
hilo atachukuliwa hatua kali za kisheria. Pia, aliwataka abiria kutolazimisha
kushushwa katika eneo hilo wakati hakuna kituo. Shio aliongeza kuwa barabara za
kuingia na kutoka Kituo cha Makumbusho bado zinakarabatiwa na Manispaa ya
Kinondoni ili kurahisisha uingiaji na utokaji wa magari katika kituo hicho.
Hivi
karibuni, madereva wa daladala zinazofanya safari kati ya Mwenge, Tegeta na
Ubungo waligoma kutoa huduma kushinikiza Serikali kueleza kituo mbadala baada
ya kufungwa kwa kituo cha Ubungo kutokana na ujenzi unaoendelea wa barabara.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SUMATRA YAFUNGA KITUO CHA DALADALA MWENGE.”
Post a Comment