Friday, May 30, 2014

SUALA LA WATENDAJI WA VIJIJI KUSOMA MAPATO NA MATUMIZI NI LA LAZIMA



Serikali imesema suala la watendaji kusoma mapato na matumizi ya vijiji ama kata ni la lazima wala si hiyari yao

Kauli hiyo imetolewa bungeni Dodoma na Naibu waziri Tamisemi Mh Agrey Mwanri katika kipindi cha maswali na majibu na kuongeza kuwa kumekuwa na mtindo wa baadhi ya watendaji wa vijiji kukataa kuwasomea wananchi mapato na matumizi wakidhani kuwa ndiyo utaratibu

Mh. Mwanri amesema ni lazima kila mtendaji wa kijiji kuwasomea wananchi wake mapato na matumizi na taarifa hiyo pia inatakiwa kubandikwa kwenye mbao za matangazo ili kila mwananchi aione kwa wakati wake

Amesema kutosoma mapato na matumizi sio tu kwamba ni kosa kisheria lakini pia linawakatisha tamaa wananchi kwa kuwa wao ndio wanachanga fedha zao na wakiona hawasomewi mapato na matumizi wanadhani kuwa fedha zao zimeliwa na wanakata tamaa ya kuchangia miradi ya maendeleo

Mh. Mwanri amesema hatua zitachukuliwa kwa watendaji wa aina hiyo ambao hawasomi mapato na matumizi kwa wananchi hao

0 Responses to “SUALA LA WATENDAJI WA VIJIJI KUSOMA MAPATO NA MATUMIZI NI LA LAZIMA ”

Post a Comment

More to Read