Friday, May 30, 2014
MWANAMKE APIGA MAGOTI HOSPITALI KUOMBA APEWE DAWA, WAUGUZI HAWAKUMSAIDIA HATIMAYE AKAFA
Do you like this story?
Unaweza
kudhani matukio haya hutokea katika hospitali za kawaida tu. Hii ni ya
kusikitisha zaidi, Picha hii ya mwisho inamuonyesha mwanamke mmoja aliyekuwa
amezidiwa hospitali na akashindwa kupatiwa dawa hadi kuamua kupiga magoti
akibembeleza apatiwe dawa ya maumivu tu kutokana na kuzidiwa kwake lakini
wauguzi hawakumsaidia chochote hadi umauti ulimkuta.
Siku
mbili baada ya kutelekezwa na maafisa wa hospitali, mwanamama huyo Margaret
Lamberty alipoteza maisha baada ugonjwa wake unaotibika kumzidi kutokana na
kushindwa kupatiwa msaada.
Margaret alifikishwa hospitali ya chuo kikuu cha A&E Kaskazini mwa Staffordshire na wanafamilia yake akiwa na maumivu makali ya tumbo, Mtoto wake kike aitwaye Laura amesema kuwa baada ya kufika hospitalini hapo wauguzi walikuwa wakimuangalia tu bila kumpa msaada wowote ndipo mama yake akaamua hadi kupiga magoti akiwaomba wampatie dawa ya maumivu lakini hakusikilizwa na mtu.

Baada ya kifo cha mwanamke huyo, Familia inapanga kuishtaki hospitali hiyo kwa kushindwa kutimiza wajibu wao hadi kusababisha kifo cha ndugu yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MWANAMKE APIGA MAGOTI HOSPITALI KUOMBA APEWE DAWA, WAUGUZI HAWAKUMSAIDIA HATIMAYE AKAFA ”
Post a Comment