Monday, May 5, 2014

MVUTANO MKALI WATOKEA BAINA YA SERIKALI NA BUNGE.




Dar es Salaam. Sasa ni dhahiri kwamba kuna msuguano wa wazi kati ya mihimili miwili ya dola, Bunge na Serikali, kuhusiana na hatua ya Serikali kuchelewa kutekeleza maazimio ya Bunge.

Msuguano huo umeshika kasi wiki hii baada ya Serikali kuwarudisha kwenye nyadhifa zao vigogo wawili wa Wizara ya Maliasili na Utalii ambao hivi karibuni waliondolewa na Waziri Lazaro Nyalandu, huku wabunge wakiapa kuibana Serikali kuwang’oa viongozi hao.

Vigogo hao ni pamoja na Mkurugenzi wa Wanyamapori, Profesa Alexander Songorwa na Mkurugenzi Msaidizi, Jaffar Kidegesho kwa madai ya kutowajibika ipasavyo katika vita dhidi ya ujangili nchini.

Mbali na sababu hiyo, lakini Nyalandu alikaririwa akisema alichukua uamuzi huo ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa mazimio 16 ya Bunge, yaliyotolewa baada ya taarifa ya Operesheni Tokomeza Ujangili.

Wakati mvutano huo ukiendelea, Ikulu imeitaka wizara hiyo kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za kumfukuza mtu kazi.

Katibu Kiongozi, Balozi Ombeni Sefue amesema kuzingatiwa sheria, kanuni na taratibu za kumfukuza mtu kazi ndiyo suluhisho la msuguano unaoendelea kati ya Waziri Nyalandu na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maliasili na Utalii, Maimuna Tarishi juu ya hatima ya wakurugenzi hao ambao walitimuliwa kazi Februari mwaka huu.

Balozi Ombeni aliwataka viongozi hao kuhakikisha kuwa uamuzi wowote wanaoufanya kuhusu kuwaondoa kazini watumishi hao unazingatia sheria, taratibu na kanuni kwa kuwa zinaeleza wazi hatua zinazopaswa kuchukuliwa.

“Siwezi kujua kwa nini wanaendelea kuvutana, hilo waulize wao, ninachojua wanatakiwa wazingatie sheria, kanuni na taratibu katika jambo hilo,” alisema.

Alipoulizwa ni nani kati ya Nyalandu na Tarishi hafuati sheria za utumishi wa umma, alisema: “We mwenyewe nenda kazisome (sheria) utajua tu.”

Kwa mujibu Sheria ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002, Kifungu cha IV (23) (2) inayozungumzia mamlaka ya Rais kumwondoa mtumishi aliyemteua kazini, amri ya kumfukuza mtumishi wa umma itatekelezwa iwapo

0 Responses to “MVUTANO MKALI WATOKEA BAINA YA SERIKALI NA BUNGE.”

Post a Comment

More to Read