Monday, May 5, 2014
MGANGA WA DIAMOND ATOBOA SIRI NZITO JUU YA TUZO 7 ALIZOPEWA, SOMA HAPA ALICHOKISEMA..! .
Do you like this story?
Yule mganga maarufu wa mastaa nchini
ambae aliwahi kutangaza kuwa amekuwa na ukaribu na mwanamuziki Diamond ameibuka
na kusema kuwa tuzo hizo saba alizozipata zinamaana kubwa sana kwenye kazi zake
anazozifanya.
Akiongea na gazeti hili kwa njia ya
simu namba 0788-844490 toka Mwanza alikoalikwa na wananchi wa huko kwa ajili ya
kutoa huduma alisema" Niliongea na Diamond wiki moja kabla ya shoo
nikamueleza kuwa atapokea tuzo nyingi sana mwaka huu na hizo tuzo ni ishara
tosha ya kudumu kwenye game kwa miaka kama hiyo ya tuzo zake kwa maana ya miaka
saba mbele yote nyota yake itaendelea kung'ara" Alisema Dokta Kamdege
Aidha Mganga huyo aliendelea
kusema" Unajuwa haya mambo ya maagano yapo muziki na miti shamba
zinaendana kwani kwenye dunia hii ya leo maadui ni wengi kuliko marafiki kwani
wapo watakaokuchukia bila sababu za msingi hivyo ni vyema ukalijua mapema hilo
na kujikinga kama ilivyo kwa Diamond" Alisema mganga huyo mwenyeji wa
Mkoa wa Tabora
Hata hivyo mganga huyo aliendelea kuto
uwito kwa watanzania popote walipo duniani waendelee kupata huduma zake kwani
hii ni kama baraka kwa taifa la Tanzania.
Dokta
Kamdege amekuwa akitumiwa sana na vigogo wa Serikali, wasanii na watu
mbalimbali duniani kufanikisha mambo yao kwa kuwapatia baraka kupitia miti
shamba
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MGANGA WA DIAMOND ATOBOA SIRI NZITO JUU YA TUZO 7 ALIZOPEWA, SOMA HAPA ALICHOKISEMA..! .”
Post a Comment