Sunday, May 25, 2014
NGOMA DAKIKA 120, REAL MADRID YAICHAPA ATLETICO MADRID 4-1 NA KUTWAA `DEBE` LA 10 LA UEFA, BALE NI KIBOKO, APIGA BAO MUHIMU MNO..
Do you like this story?
Gareth Bale aliifungia bao muhimu Real Madrid katika fainali ya UEFA. |
Bale akinyanyua kombe la UEFA |
Nahodha Iker Casillas akinyanyua kombe |
Ronaldo na Bale wakifurahia ushindi wa Real Madrid |
HATIMAYE Gareth Bale ameisaidia Real Madrid kutumiza ndoto za `La Decima` baada ya kutwaa ndoo ya 10 ya UEFA kufuatia ushindi wa dakika za nyongeza katika mchezo wa fainali dhidi ya majirani zao Atletico Madrid.
Alizaliwa Wales, alikulia Southampton na kung`ara Tottenham, nyota huyo mwenye miaka 24 ameendelea kuonesha kuwa Real Madrid hawakukosea kumsajili kwa rekodi ya dunia baada ya kufunga bao ambalo limeandikwa katika historia ya klabu.
Bale alionekana kutokuwa makini kipindi cha kwanza baada ya kupoteza nafasi za kufunga, lakini aliendeleza rekodi nzuri ya msimu wake wa kwanza Real Madrid baada ya kuifungia bao la pili katika dakika za nyongeza, kabla ya vijana hao wa Carlo Ancelotti kushinda kwa mabao 4-1.
Kikosi
cha Real Madrid: Casillas, Carvajal, Varane, Sergio
Ramos, Fabio Coentrao (Marcelo 59), Modric, Khedira (Isco 59), Di Maria, Bale,
Benzema (Morata 79), Ronaldo.
Wachezaji wa akiba: Diego Lopez, Pepe, Arbeloa, Illarramendi.
Wachezaji wa akiba: Diego Lopez, Pepe, Arbeloa, Illarramendi.
Waliopata kadi za njano: Ramos, Khedira, Marcelo, Ronaldo, Varane.
Waliofunga magoli. Ramos 90, Bale 110, Marcelo 118, Ronaldo 120.
Kikosi cha Atletico Madrid: Courtois, Juanfran, Miranda, Godin, Filipe Luis (Alderweireld 83), Raul Garcia (Sosa 66), Gabi, Tiago, Koke, Villa, Diego Costa (Adrian 9).
Wachezaji wa akiba: Aranzubia, Mario Suarez, Rodriguez, Diego.
Mfungaji wa Goli: Godin 36.
Walioneshwa kadi nyekundu: Garcia, Miranda, Villa, Juanfran, Gabi, Koke, Godin.
Mwamuzi: Bjorn Kuipers (Holland)
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NGOMA DAKIKA 120, REAL MADRID YAICHAPA ATLETICO MADRID 4-1 NA KUTWAA `DEBE` LA 10 LA UEFA, BALE NI KIBOKO, APIGA BAO MUHIMU MNO..”
Post a Comment