Saturday, May 24, 2014
CECAFA NILE BASIN CUP: THEM FELIX `MNYAMA` ATIKISA NYAVU MBEYA CITY FC IKIIBAMIZA 3-2 ACADEMIE TCHITE YA BURUNDI
Do you like this story?
UNAKUMBUKA ule moto wa Mbeya City
katika michuano ya ligi kuu soka Tanzania bara msimu uliopita?.
Wawakilishi hao wa Tanzania
wamehamishia kasi yao katika michuano mipya ya CECAFA Nile Basin Cup, ambapo
wameanza vyema mashindano hayo baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi
ya Academie Tchite ya Burundi.
Mabao ya Mbeya City yamefungwa na
washambuliaji hatari Paul Nonga katika
dakika ya 15, Mwegane Yeya dakika ya 27 na nyota mpya Them Felix katika dakika
ya 37.
Mechi hiyo muhimu kwa Mbeya City fc
iliyosuasua kuwasili Sudan kutokana na kucheleweshewa tiketi za ndege imepigwa
katika uwanja wa Khartoum-Sudan.
Kikosi cha
Mbeya City kilichoanza leo ni Barhan David, Kabanda John, Kibopile Hamad,
Julius Deogratius, Yohana Morris, Antony Matogolo, Deus Kaseke, Mazanda Steven,
Paul Nonga, Mwegane Yeya na Them Felix `Mnyama`.
Mbali na
mchezo wa Mbeya City fc, majira ya saa 2:00 usiku AFC Leopard ya Kenya
itakabiliana na Enticelles ya Rwanda.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “CECAFA NILE BASIN CUP: THEM FELIX `MNYAMA` ATIKISA NYAVU MBEYA CITY FC IKIIBAMIZA 3-2 ACADEMIE TCHITE YA BURUNDI”
Post a Comment