Saturday, May 24, 2014
BAADA YA KUTEMWA KIKOSI CHA BRAZIL, RONALDINHO AAMUA KUPANGISHA NYUMBA YAKE YA RIO de JANEIRO, KODI HIYO mhhhhh!
Do you like this story?
BAADA ya
kuachwa katika kikosi cha Luiz Felipe Scolari kitakachoshiriki kombe la
dunia katika ardhi ya nyumbani, Ronaldinho `Gaucho` amebuni njia mpya ya
kuingiza mkwanja kwenye mashindano ya kombe la dunia yanayoanza majira ya
kiangazi mwaka huu.
Mshambuliaji
huyo wa zamani wa Barcelona ameamua kupangisha nyumba yake iliyopo mjini Rio de
Janeiro kwa kodi ya Euro 9, 120 kwa usiku mmoja, lengo likiwa ni kuwapa
mashabiki fursa ya kula bata kwenye mjengo wa gwiji huyo wa Brazil.
Ronaldinho
aliandika katika mtandao wake wa Twita kuthibitisha kuwa nyumba yake yenye
vyemba vitano ipo tayari kwa ajili ya kupangishwa wakati wa mashindano na kama
mtu anahitaji anatakiwa kufanya `mambo` kupitia tovuti ya Airbnb.com.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “BAADA YA KUTEMWA KIKOSI CHA BRAZIL, RONALDINHO AAMUA KUPANGISHA NYUMBA YAKE YA RIO de JANEIRO, KODI HIYO mhhhhh!”
Post a Comment