Thursday, May 15, 2014
NYOTA WA TANZANIA, MBWANA SAMATTA NA THOMAS ULIMWENGU KUTUA DAR JUMAMOSI KUICHEZEA TAIFA STARS DHIDI YA ZIMBABWE
Do you like this story?
RAIS wa shirikisho la soka nchini
Tanzania, Jamal Malinzi imepigana kiume kuwasiliana na mwenyekiti na mmiliki wa
klabu ya TP Mazembe, Moise Katumbi na
taarifa njema juu ya mawasiliano hayo ni kwamba washambuliaji wawili wa
kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta na Thomas Ulimwengu watawasili
jumamosi mchana kwa ajili ya mchezo wa jumapili.
Taarifa za uhakika kutoka ndani ya TFF
zinaeleza kuwa Rais Malinzi amethibitisha ujio wa wanandinga hao tegemeo kwa
Taifa stars na kuibua matumaini ya Taifa stars kufanya vizuri kwasababu Samatta
na Ulimwengu ni wachezaji mahiri zaidi kwa sasa.
Nyota hao wawili watatumiwa kwa mara ya
kwanza na kocha wa Taifa stars, Mart Nooij katika mechi ya raundi ya awali
kuwania kufuzu fainali za mataifa ya Afrika mwakani nchini Morocco dhidi ya
Zimbabwe kwenye uwanja wa Taifa, jijini Dar es salaam.
TP Mazembe aliwazuia wachezaji hao kuja
Tanzania kwasababu wanawahitaji katika michezo ya makundi ya ligi ya mabingwa
barani Afrika.
Matajiri hao wa DRC walipo kundi A wanatarajia kucheza mechi ya kwanza dhidi ya El Hilal Omduran siku ya ijumaa mjini
Khartoum nchini Sudan, hivyo baada ya mechi hiyo wachezaji hao wa Tanzania
watatua nchini jumamosi na kucheza mechi siku ya jumapili.
Hata hivyo baada ya mechi hiyo watakwea
pipa kuelekea Lubumbashi DRC tayari kwa maandalizi ya mechi ya pili dhidi ya mahasimu
wao AS Vita mei 25 mwaka huu.
Baada ya mechi hiyo na AS Vita ambapo
wiki iliyopita walikutana nao katika mchezo wa mwisho wa ligi kuu ya DRC na
kushuhudia vurugu kubwa ziliosababisha watu zaidi ya 15 kupoteza maisha,
Samatta na Ulimwengu wataweza kupata nafasi ya kucheza mechi ya marudiano na
Zimbabwe mjini Harare.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “NYOTA WA TANZANIA, MBWANA SAMATTA NA THOMAS ULIMWENGU KUTUA DAR JUMAMOSI KUICHEZEA TAIFA STARS DHIDI YA ZIMBABWE”
Post a Comment