Friday, May 9, 2014
PATA MKWANJA PATA MKWANJA KAZI KWAKO KAZI KWAKO OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI NCHINI.
Do you like this story?
Ofisi ya
Taifa ya Takwimu imeeleza kuwa mfumuko wa bei nchini kwa mwezi
Aprili umeongezeka ikilinganishwa na mwezi uliopita kutokana na kupanda kwa bei
za bidhaa na huduma mbalimbali.
Akizungumza
na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam Mkurugenzi wa Takwimu za Jamii
na sensa ya Watu na Makazi Bw. Ephraim Kwesigabo amesema kuwa mfumuko wa bei wa
Taifa kwa mwezi Aprili 2014 umeongezeka na kufikia asilimia 6.3 kutoka asilimia
6.1 za mwezi uliopita.
Amesema kasi
ya upandaji wa bei za bidhaa na huduma mbalimbali kwa mwezi Aprili 2014
imeongezeka kidogo ikilinganishwa na ile iliyokuwepo mwezi Machi huku
kukiwa na ongezeko dogo la upandaji wa bei kwenye baadhi ya bidhaa na
huduma kwa mwezi huu ikilinganishwa na bei za mwezi uliopita.
Ameeleza
kuwa mfumuko wa bei za bidhaa za vyakula na migahawa kwa mwezi Aprili
umeongezeka hadi asilimia 8.5 kutoka asilimia 7.9 za mwezi Machi mwaka huu na
kuongeza kuwa bei za bidhaa za vyakula na vinywaji baridi imeongezeka hadi
asilimia 7.8 kutoka asilimia 7.2 za mwezi uliopita huku badiliko la fahirisi za
bidhaa zisizo za vyakula likipungua hadi asilimia 4.9 kwa mwezi Aprili 2014
kutoka asilimia 7.2 iliyokuwepo mwezi uliopita.
Kwa upande wa
mfumuko wa bei unaopimwa kwa kipimo cha mwezi,amefafanua kuwa
kumekuwa na ongezeko dogo la asilimia 0.7 ikilinganishwa na ongezeko la
asilimia 0.6 kwa lililokuwepo mwezi Machi mwaka huu, huku fahirisi za bei
za taifa zikiongezeka hadi kufikia 150.50 kwa mwezi Aprili 2014 kutoka 149.49
za mwezi Machi.
Amezitaja
bidhaa zilizochangia ongezeko la fahirisi za bei nchini kuwa ni pamoja na
mchele, mahindi,unga wa Muhogo,Kuku wa kienyeji, dagaa,samaki wakavu, matunda,
karanga na mihogo.
Kwa upande wa
bidhaa zisizo za vyakula zilizochangia ongezeko la fahirisi amesema ni pamoja
mkaa wa kupikia, huduma za matibabu, mafuta ya dizeli,na gharama ya kusaga
nafaka.
Kuhusu
uwezo wa shilingi 100 ya Tanzania katika kununua bidhaa na huduma kwa mwezi
Aprili Bw. Kwesigabo amesema kuwa umepungua na kufikia shilingi
66 na senti 45.
“Kupungua kwa
thamani ya Shilingi kunamaanisha kwamba, kama mtu alikuwa na uwezo wa kununua
bidhaa kwa Shilingi 100 kwa mwaka jana, kwa kipindi hiki itampasa aongeze zaidi
ili aweze kununua kitu kama kile kile mfano badala ya shilingi 100 inabidi
atumie shilingi 134”
Kuhusu
ulinganifu mfumuko wa bei wa Tanzania na baadhi ya nchi za Afrika
Mashariki amesema kuwa una mwelekeo unaofanana na kueleza kuwa mfumuko wa bei
nchini Kenya umeongezeka na kufikia asilimia 6.41 kwa mwezi Aprili 2014
kutoka asilimia 6.27 za mwezi Machi , huku Uganda ikiwa na mfumuko
wa asilimia 6.7 kwa mwezi huu ikilinganishwa na 7.1 za mwezi uliopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ PATA MKWANJA PATA MKWANJA KAZI KWAKO KAZI KWAKO OFISI YA TAIFA YA TAKWIMU YATOA TAARIFA YA MFUMUKO WA BEI NCHINI.”
Post a Comment