Wednesday, May 7, 2014

PICHA NA TAARIFA KUHUSU MAJERUHI ALIYELIPUKIWA NA BOMU KANISANI JIJINI MWANZA.


Picha kutoka maktaba



Mtu mmoja amenusurika kufa baada ya kulipukiwa na bomu lili lotengenezwa kienyeji kisha kuhifadhiwa katika mfumo wa zawadi na kutegwa katika nyumba ya kupumzikia wageni iliyopo kanisani la Kiinjili la Kilutheri Tanzania KKKT jijini Mwanza usiku wa kuamkia leo.
 
Majeruhi huyo ambaye ni mhudumu wa nyumba hiyo Benadeta Alfred amelazwa katika hospitali ya Rufaa Bugando ambapo anapatiwa matibabu baada ya kujeruhiwa vibaya sehemu kubwa ya mwili wake
 
Kutokea kwa mlipuko huu wa  bomu katika eneo hili la kanisa kunaacha maswali mengi kwa wakazi wa jiji la Mwanza
Bomu hili lilowekwa kwa mfumo wa zawadi ndani ya nyumba ya kupumzikia linadaiwa kuwa hapa kwa mda wa siku tatu bila kufahamu mwenye mzigo huu na kilichomo ndani yake
 
Licha ya uimara wa fensi na ulinzi uliopo katika eneo hili la kanisa maswali mengi yanaibuka juu ya mhusika aliyeingiza bomu hilo na kwa njia gani.

Kikosi maalum cha uchunguzi wa milipuko kimewasili kutoka jijini Dar es salaam kufanya uchunguzi katika eneo hili la mlipuko.
 
Aidha wito umetolewa kwa wananchi wote kuwa makini na vitu wasivyovijua ili kujiepusha na madhara kama haya.
 
Juhudi za kunusuru maisha ya Benardeta zinaendelea hapa katika hosptali ya rufaa ya Bugando katika chumba cha ungalizi maalumu.
 
Matukio ya milipuko inayosadikiwa kuwa mabomu imeendelea kurindima nchini hasa katika mikoa ya Arusha, visiwani Zanzibar na sasa jijini Mwanza, hali ambayo inaacha swali kwa jeshi la polisi juu ya usalama wa raia katika maeneo yasio rasmi na ya umma.

0 Responses to “PICHA NA TAARIFA KUHUSU MAJERUHI ALIYELIPUKIWA NA BOMU KANISANI JIJINI MWANZA.”

Post a Comment

More to Read