Wednesday, May 7, 2014
WALIOKUFA KWA KUNYWA POMBE HARAMU "CHANG'AA" HUKO KENYA SASA NI ZAIDI YA 50,ZAIDI YA MIA MOJA WAMELAZWA.
Do you like this story?
Pombe Haramu au
Chang'aa kama inavyojulikana nchini Kenya
Watu zaidi ya hamsini
na tano wamefariki katika maeneo mbali mbali nchini Kenya baada ya kunywa pombe
'haramu'.
Maeneo hayo yako katika mkoa wa kati na
katika eneo la Mashariki mwa Kenya.
Maeneo hayo ni pamoja na majimbo ya
Kiambu ambako watu 15 wamefariki, Jimbo la Embu Mashariki mwa nchi ambako
wengine zaidi ya 20 wamefariki.
Katika majimbo ya Kitui na Makueni
mashariki mwa Kenya watu 20 wameripotiwa kufariki.
Vifo hivyo vilitokea kuanzia Jumapili
siku ambayo watu zaidi ya miamoja walibugia pombe haramu inayosemekana ilikuwa
imechanganywa na kemikali aina ya Methanol ambayo ni sumu kwa mwili.
Inaarifiwa wengine zaidi ya miamoja
wamelazwa hospitalini baada ya kubugia pombe hiyo haramu siku ya Jumapili,
baadhi wakiwa katika hali mahututi huku wengine wakiwa wamepoteza uwezo wao wa
kuona.
Watu hao inashukiwa walikunywa mvinyo
ambao ulikuwa umechanganywa na kemikali ya Methanol.
Mwanamume mmoja ambaye alienda ulevini
na mkewe alisema kuwa mke wake alianza kwa kupoteza uwezo wake wa kuona na
kisha kufariki muda mfupi baadaye.
Wengi waliofikishwa hospitalini
walikuwa wanaumwa na tumbo, wanahisi kisunzi na kuumwa na kichwa. Wengine
walifikishwa hospitalini wakiwa katika hali mahututi na kufariki wakipokea
matibabu.
Shirika la kupambana na utumiaji wa
pombe na madawa ya kulevya, NACADA limesema kuwa wale waliohusika katika uuzaji
na usambaji wa pombe hiyo watachukuliwa hatua kali za kisheria.
Vita dhidi ya pombe haramu nchini Kenya
vimekuwa vigumu kushinda kwani watu wenye kipato cha chini huchagua kutumia
pombe ya bei nafuu ambayo huwa sio pombe halali na kukabiliwa na hatari kama
hizi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WALIOKUFA KWA KUNYWA POMBE HARAMU "CHANG'AA" HUKO KENYA SASA NI ZAIDI YA 50,ZAIDI YA MIA MOJA WAMELAZWA.”
Post a Comment