Wednesday, May 7, 2014
UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WATENGEWA SH 5 BILIONI.
Do you like this story?
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda jana aliwasilisha bungeni, bajeti ya ofisi yake na mfuko wa
Bunge inayofikia Sh5.21 trilioni. Kati ya hizo, Sh5 bilioni zimetengwa kwa
ajili ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliopangwa kufanyika baadaye mwaka huu.
Hayo
yalielezwa bungeni jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Tamisemi),
Hawa Ghasia wakati wa maelezo kuhusu kazi zilizotekelezwa mwaka 2013/2014 na
mwelekeo wa kazi zitakazotekelezwa 2014/2015.
Ghasia
amesema shughuli zitakazogharimiwa na fedha hizo ni pamoja na maandalizi ya
masanduku ya kupigia kura, kupitia kanuni za uchaguzi na kuandaa fomu na
nyaraka mbalimbali za uchaguzi.
Shughuli
nyingine ni uhakiki wa majimbo ya uchaguzi huo ambayo ni vijiji, mitaa na
vitongoji.
Katika
bajeti hiyo ya Ofisi ya Waziri Mkuu, Sh132.6 bilioni zimetengwa kwa ajili ya
Mfuko wa Bunge la Muungano, kati yake posho na mishahara kwa ajili ya Bunge
(wabunge na watumishi wa Bunge) ikiwa ni Sh123.94 bilioni.
Kwa
mujibu wa nyaraka za bajeti hiyo, wabunge peke yao wametengewa Sh102.317
bilioni kwa ajili ya mishahara, posho za vikao na kujikimu na posho za safari
ndani na nje ya nchi.
Kwa
mwaka wa fedha unaomalizika Juni 30 mwaka huu, mishahara na posho za wabunge
zilitengwa Sh93.37 bilioni, kati ya hizo posho zilikuwa Sh48.74 bilioni
ikilinganishwa na Sh49.526 bilioni zilizotengwa katika bajeti 2014/2015, sawa
na ongezeko la Sh800 milioni.
Usimamizi
wa rasilimali watu na utawala ambayo ndiyo inayohusika na mishahara na posho
kwa watumishi wa Bunge kwa mwaka wa fedha wa 2014/2015, umetengewa Sh21.6
bilioni.
Takwimu
hizo zinaonyesha kuwa mishahara ya wabunge imetengewa Sh12.769 bilioni.
Posho
za safari ndani ya nchi zimetengewa Sh11.192 bilioni wakati zile za safari za
nje kwa wabunge zimetengewa Sh9.08 bilioni.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA WATENGEWA SH 5 BILIONI.”
Post a Comment