Thursday, May 15, 2014
POLISI WAMGUNDUA KINARA WA MTANDAO WA WIZI KATIKA MABENKI JIJINI D’SALAAM, PICHA ZAKE HIZI HAPA
Do you like this story?
Kamishna kova leo alipoamua kuitoa hadharani picha ya mtuhumiwa huyo mbele ya wanahabari ili apatikane mara moja |
RONALD S/O MOLLEL ambaye ndiye mtuhumiwa wa ujambazi katika mabenk mbalimbali hapa jijini dar es salaam |
Endapo utamona mtu huyu toa ripot mahali popote hata kwa mmiliki wa blog hii |
Jeshi la
Polisi Kanda Maalum D’Salaam limefanikiwa kumbaini mtuhumiwa mhimu ambaye ni
kinara wa mtandao wa wizi katika mabenki ambaye anajulikana kwa jina la RONALD
S/O MOLLEL umri miaka 37, mfanyabishara na mkazi wa Kimara Bonyokwa Jijini
D’salaam.
Mtuhumiwa
huyu amekimbilia mafichoni mara baada ya tukio la ujambazi katika Tawi la Benki
ya Barclays Kinondoni lililotokea tarehe 15/4/2014 ambapo majambazi
walifanikiwa kupora kiasi kikubwa cha fedha T.Shs.390,220,000/= , USD 55,000/=
na EURO 2150/=.
Aidha sasa imefahamika kwamba mtuhumiwa huyu ni mume wa
mtuhumiwa wa kwanza katika tukio la Barclays Benki aitwaye ALUNE D/O KASILILIKA
@ ALUNE D/O MOLLEL , miaka 28, Mkazi wa Kimara Bonyokwa ambaye ni Meneja
wa Benki Tawi la Barclays Kinondoni. Mtuhumiwa Mollel anatafutwa kwa kila
hali kwa vile yeye ndiye alikuwa kinara wa kupanga tukio hilo la Barclays na
mara baada ya tukio ametoroka na kiasi kikubwa cha fedha hizo zilizoibiwa.
Zipo taarifa
za kuaminika kuwa mtuhumiwa huyu amekuwa akipanga na kushiriki kikamilifu
katika matukio mbali mbali ya uhalifu mkubwa ikiwa ni pamoja na kuongoza
vikundi vya majambazi vilivyowahi kupora katika mabenki mbali mbali katika
kipindi cha mwaka mmoja uliopita. Mtuhumiwa huyo ni hatari kwani ana
mtandao na watumishi muhimu katika matawi mbali mbali ya mabenki kwa lengo la
kufanikisha uhalifu katika mabenki hayo.
Jeshi la
Polisi limelazimika kutoa picha yake hadharani kwa kutumia dhana ya ulinzi
shirikishi ili mtuhumiwa huyu akionekana akamatwe na taarifa zitolewe katika
kituo chochote cha Polisi ikiwa ni lengo la polisi kupambana na uhalifu katika
dhamira ya kuzuia uhalifu, kulinda maisha na mali za wananchi.
Zawadi nono
ya fedha taslim itatolewa kwa siri kwa mtu yeyote atakayetoa taarifa
zitakazosaidia kukamatwa kwa mtuhumiwa huyu. Pamoja na maelezo hayo
mtuhumiwa mwenyewe sasa anapewa fulsa ya kujisalimisha katika kituo chochote
cha polisi kabla ya kukamatwa kwa njia nyingine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “POLISI WAMGUNDUA KINARA WA MTANDAO WA WIZI KATIKA MABENKI JIJINI D’SALAAM, PICHA ZAKE HIZI HAPA ”
Post a Comment