Thursday, May 1, 2014
RATIBA KUTATIZA KOMBE LA AFRIKA 2015.
Do you like this story?
Shirikisho
la soka duniani FIFA limesema kuwa vilabu havitashurutishwa kuwaachilia
wachezaji wao ili washiriki mechi za kufuzu kwa michuano ya kombe la taifa
bingwa Afrika mwaka 2015.
Hii
ni kwa sababu tarehe ya kufanyika kwa michuano hiyo iko nje ya tariba ya
shirikisho hilo ya michuano ya kimataifa.
Hii
huenda ikasababisha mgongano kati ya vilabu na nchi hasa ikizingatiwa mechi za
ufunguzi zinazogongana na mechi za vilabu barani Afrika.
Mechi
za taifa bingwa Afrika, shirikisho na kombe la klabu bingwa Ulaya itafanyika
kati ya tarehe 16-17.
Mechi
hizo hazipo kwenye ratiba ya FIFA na kwa hivyo haitakuwa lazima wachezaji wa
vilabu kuruhusiwa kuondoka.
Hata
hivyo, michuano ya makundi itakayoshirikisha Ghana, Nigeria na Cameroon,
zitakuwa katika tarehe iliyoidhinishwa na FIFA , ikimaanisha kuwa vilabu vya
soka kote duniani lazima viwaruhusu wachezaji wao kushiriki mechi hizo.
Wachezaji
kama Edward Sadomba, wataathiriwa na mgongano wa tarehe zilizo kati ya mechi za
kufuzu zitakazofanyika 2015 na michuano ya vilabu.
Sadomba
atahitajika kwa wakati mmoja na klabu yake ya Al Ahli Benghazi pamoja na timu
yake ya taifa Zimbabwe.
Ni
hali sawa kwa mchezaji wa Zamalek kutoka Mauritania Dominque da Silva pamoja na
mtanzania Mbwana Samatta, anayechezea TP Mazembe ya DR Congo.
Maafisa
wa kombe la mashirikisho wamesema kuwa wataviandikia barua vilabu vyenye
wasiwasi wakitaka wachezaji kuruhusiwa kuwakilisha nchi zao kwa sababu ya
changamoto zinazotokana na ratiba.
Lakini
FIFA imesema kuwa wachezaji wanaweza tu kuondoka ikiwa
maafisa wa vilabu na mashirikisho ya nchi husika wanaweza kukubaliana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “RATIBA KUTATIZA KOMBE LA AFRIKA 2015.”
Post a Comment