Wednesday, May 21, 2014
VITA VITANI! SAMUEL ETO`O AMZABA KIBAO KINGINE JOSE MOURINHO JUU YA UMRI WAKE
Do you like this story?
Achana na mimi: Samuel Eto'o alimshambulia kocha wa Chelsea Jose Mourinho baada ya kuambiwa amezeeka. |
Mapema mwezi huu, Mourinho alipachikwa jina la `Mjinga` na Mcameroon, Samuel Eto`o |
KWA mara
nyingine tena, Mcameroon, Samuel Eto'o ametengeneza vichwa vya habari
kwenye magazeti baada ya kumshambulia kocha wa Chelsea Jose Mourinho juu
ya umri wake.
Katika
mahojiano yake na Tovuti ya shirikisho la Soka la Kiafrika, nyota huyo mwenye
miaka 33 amemtaja Mourinho kama `Mnafiki` baada ya awali kumuelezea Mreno huyo
kuwa ni `mjinga` .
Kitendo
cha Eto`o kuendeleza vita ya maneno na bosi wake kinadhihirisha kuwa Eto`o sasa
anaondoka Stamford Bridge.
Eto'o,
aliyeshinda taji la UEFA chini ya Mourinho katika klabu ya Inter Milan,
aliwaambia cafonline.com:
"Kinyume
na maneno ya `mnafiki` juu ya umri wangu, bado niko fiti kiuchezaji".
"Kwa
miaka 33, bado najiona kuwa fiti. Nimethibitisha hilo kuwa naweza kufanya
vizuri zaidi ya vijana".
Mourinho
alinaswa na Camera akisema maneno mabaya kwa Eto`o kuwa umri wa nyota huyo
unaweza kuwa zaidi ya umri wake halisi.
Eto'o,
ambaye aliifungia Chelsea magoli 12 alishangilia moja ya bao lake
kwa staili ya kibabu kinachotembelea mkongojo na kurudia kuwa bado anao uwezo
wa kuendelea kucheza ligi za barani Ulaya.
"Napenda
kusema kuwa siendi Marekani wala mashariki ya mbali," alisema Eto`o ambaye
amemaliza mkataba wake wa mwaka mmoja aliosaini katika klabu ya Chelsea
akitokea Anzhi Makhachkala.
"Nitaendelea
kucheza `levo` za juu. Nitaendekea kucheza ligi ya mabingwa. Bado nina
mapenzi makubwa na mashindano haya".
"Sitawaambieni
ni wapi, lakini bado nitakuwa `levo` za juu. Nina miaka 33 na bado nina
makombe mawili ya dunia sijacheza".
"kabla
yangu mimi kuna wachezaji waliocheza mpaka miaka 41. Kwahiyo namimi
naweza".
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “VITA VITANI! SAMUEL ETO`O AMZABA KIBAO KINGINE JOSE MOURINHO JUU YA UMRI WAKE”
Post a Comment