Tuesday, June 3, 2014
03 Jun 2014 MTOTO MCHANGA AOKOTWA AKIWA AMEKUFA, ALIZIBWA PUANI NA MDOMONI KWA PLASTA ILI ASIPIGE KELELE
Do you like this story?
Pamoja na jitihada kubwa inayofanywa na
serikali katika kupambana na matukio ya ukatili kwa watoto, bado jamii
inaonekana haijaipata elimu hiyo kutokana na kuendelea kuwepo kwa matukio hayo.
Leo mtoto mchanaga anayekadiliwa kuwa
na umri wa siku moja amekutwa akiwa ametupwa eneo la Mbuyuni Kawe huku akiwa
amefungwa plasta sehemu ya mdomoni na puani kumzuia kutopiga kelele pamoja na
kuvuta pumzi.
Bw. Khamisi Hamad Bundala ambaye ni
mvuvi katika eneo la Kawe, alisema tukio hilo walilijua mara baada ya mwenzao
(pia mvuvi) kwenda kwenye eneo la tukio kwa ajili ya kuokota mfuko wa Rambo kwa
nia ya kuwekea samaki na kisha kumkuta mtoto huyo ndani ya mfuko.
“Sasa baada ya kufika pale mbuyuni na kutaka
kuuchukuwa mfuko wa Rambo ndio akaona kile kitoto na ndipo alipotuita na sisi
na kushuhudia tukio hili. Kiukweli ni tukio baya sana na linalopaswa kupingwa
na kila mmoja wetu, huu ni ukatili mbaya sana,” alisema .
“Polisi ifanye kila linalowezekana
kukamatwa kwa huyo mama kiukweli huu ni zaidi ya ukatili,” alisema Edna Hamad
mkazi wa Kawe.
Aidha, polisi wa kituo cha Kawe
walifika na kuuchukuwa mwili wa mtoto huyo.
Jitihada na kumpata Kamanda wa polisi
mkoa wa kipolisi Kinondoni Bw. Camilius Wambura kwa ajili ya kuzungumzia tukio
hilo hazikuzaa matunda baada ya simu yake ya mkononi kutopatikana.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “ 03 Jun 2014 MTOTO MCHANGA AOKOTWA AKIWA AMEKUFA, ALIZIBWA PUANI NA MDOMONI KWA PLASTA ILI ASIPIGE KELELE”
Post a Comment