Tuesday, June 3, 2014
FRENK LAMPARD KUAGA CHELSEA.
Do you like this story?
Kiungo cha kati wa Chelsea Frank Lampard ametangaza kwamba ataondoka
katika klabu hiyo baada ya kuichezea kwa miaka 13.
Mchezaji
huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 35 na ambaye ndiye mfungaji bora zaidi
wa mabao katika klabu hiyo kwa jumla ya mabao 211, anamaliza kandarasi yake
mwezi huu.
Tangu
alipojiunga na klabu hiyo kutoka West Ham mwaka wa 2001, Lampard ameshinda
mataji makuu 11, zikiwemo 3 za ligi ya Premier na ile ya vilabu bingwa mwaka wa
2012.
''Klabu
hii imekuwa sehemu ya maisha yangu,” amesema Lampard ambaye anaweza kustaafu
ingawa vilabu 16 vinataka kumsajili.
Sasa
hivi yuko pamoja na kikosi cha Uingereza mjini Miami kabla ya Kombe la Dunia na
hatafanya uamuzi wowote kuhusu hatima yake baada ya mashindano hayo.
Baada
ya kusajiliwa kwa Euro milioni 11, Lampard aliichezea Chelsea michuano 688 na
kumfanya kuwa mchezaji wa tatu kuwahi kuichezea klabu hiyo mechi nyingi zaidi
nyuma ya Ron Harris aliyecheza mechi 795 na Peter Bonetti aliyecheza mechi 729.
Katika
muda wake kwenye klabu hiyo iliyoko magharibi mwa London, amewahi pia kushinda
mataji 4 ya FA, mawili ya ligi na ligi ya Uropa.
''Nilipojiunga
na klabu hii nzuri miaka 13 iliyopita, singewahi kuamini kwamba ningekuwa
mwenye bahati ya kucheza mechi nyingi na kushiriki ufanisi namna hii,”
aliongezea Lampard, mchezaji bora wa mwaka wa Chelsea mara tatu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “FRENK LAMPARD KUAGA CHELSEA.”
Post a Comment