Sunday, June 22, 2014
HODGSON AMUOMBA GERRARD KUICHEZEA ENGLAND FAINALI ZA ULAYA 2016
Do you like this story?
Luis Suarez akimpa pole Gerrard baada ya kufanya vibaya kombe la dunia |
Hodgson ana matumaini ya kutompoteza Gerrard. |
ROY
Hodgson atajaribu kumshawishi Steven Gerrard ili aendelee kucheza
soka la kimataifa mpaka 2016.
Nyota huyo
amebaki njia panda juu ya hatima ya soka lake la kimataifa kutokana na matokeo
mabaya ya kombe la dunia, lakini bado anahitajika na klabu yake ya Liverpool
itakayoshiriki michuano ya UEFA msimu ujao.
Japokuwa
Gerrard, 34, ameshindwa kutamba kombe la dunia, thamani yake na uzoefu wake
unahitaji katika kikosi cha England na Hodgson anatamani kuona anaendelea
kucheza licha ya vijana wengu kuchipukia kwasasa.
Frank
Lampard anajiandaa kustaafu soka la kimataifa, kwahiyo Gerrard atabaki mchezaji
pekee mkongwe na England haitaki kumpoteza kwasababu anawaunganisha vijana
katika kikosi hicho.
Hata
hivyo, Gerrard ataifikiria klabu yake ambayo ina mechi ngumu msimu ujao baada
ya kufuzu UEFA.
Gerrard
amesema atafanya maamuzi baada ya kuzungumza na marafiki, familia na kocha wa
Liverpool, Brendan Rodgers baada ya kombe la dunia.
Mawazo
Rodgers yatakuwa muhimu zaidi na inaonekana kocha wa Liverpool na madaktari wa
timu watapenda kumpa mapumziko Gerrard baada ya kombe la dunia.
Hata kama
mwenyekiti wa FA , Greg Dyke amemhakikishia kazi Hodgson mpaka 2016
licha ya kuchemsha kombe la dunia, mechi ya mwisho dhidi ya Costa Rica itakuwa
muhimu sana na kama England itapoteza, kocha huyo atakuwa katika mazingira
mabaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HODGSON AMUOMBA GERRARD KUICHEZEA ENGLAND FAINALI ZA ULAYA 2016”
Post a Comment