Sunday, June 22, 2014
UGANDA YAITUNISHIA MISULI MAREKANI KUHUSU USHOGA
Do you like this story?
Katibu mkuu wizara ya mambo ya nje wa
Uganda, Balozi James Mugume, amesema kuwa Uganda haitishwi na vikwazo
ilivyowekewa na Marekani kama hatua ya kupinga sheria yake kali kuhusu Ushoga.
Kwa mujibu wa BBC, Balozi Mugume
ameelezea kuwa serikali ya Uganda hata hivyo itafanya mazungumzo na Marekani
ili kufafanua hatua waliyochukua.
Amesisitiza kuwa wataieleza Marekani
sheria hiyo inapinga tabia ambayo sio ya kiafrika na maadili ambayo
hayakubaliki katika jamii nyingi za kiafrika.
Serikali imesisitiza kuwa vikwazo hivyo
havitakuwa na athari kubwa kwa nchi hiyo na pia imekanusha madai ya mashirika
ya kijamii kuwa tayari sheria hiyo imechochea ongezeko la dhuluma dhidi ya
wapenzi wa jinsia moja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “UGANDA YAITUNISHIA MISULI MAREKANI KUHUSU USHOGA ”
Post a Comment