Friday, June 20, 2014
MTU ANAYEMILIKI AKAUNTI YA TWITTER YA AL SHABAAB AKAMATWA NCHINI KENYA.
Do you like this story?
Maafisa wa polisi wa Kenya wamemtia
nguvuni mshukiwa anayetuhumiwa kuendesha akaunti ya Twitter ambayo ina uhusiano
na kundi la kigaidi la Al shabaab na uliotoa habari kwamba Al shabaab
walihusika kutekeleza mauaji eneo la Mpeketoni kaunti ya Lamu.
Kwa mujibu wa Ripota Julius
Kepkoech toka Kenya, Katibu wa wizara ya Mambo ya ndani na usalama
wa taifa, Mutea Iringo amethibitisha kwamba Ismail Omondi ametiwa nguvuni
Tarehe 18 June mwaka huu ambapo hata hivyo Iringo amekanusha kwamba mshukiwa
huyo hana uhusiano wowote na Al Shabaab.
Iringo amesema, “Unaweza kuona
kwamba yule anayekiri kuhusika na Alshabaab si mmoja wa kiongozi wa kundi
hilo,”.
Inspekta Jenerali wa Polisi David
Kimaiyo awali amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter kwamba: “Aliye
kizuizini kwa sasa ni mshukiwa anayeendesha mtandao wa kijamii unaodhaniwa
kutumiwa na Al shabaab kukiri kuhusika na uvamizi”
Hata hivyo Kimaiyo hakutoa taarifa
zaidi kuhusiana na washukiwa.
Ismail Omondi ni mshukiwa wa tatu
kutiwa nguvuni kuhusiana na mauaji yaliyotokea Mpeketoni siku ya Jumapili na
Jumatatu ambapo zaidi ya watu 60 wamepoteza maisha.
Mapema siku ya Jumatano, mshukiwa
mwingine Ahmed Abdallah anayetuhumiwa kumiliki gari lililowabeba wavamizi hao
alikamatwa huku Salim Dyana naye akikamatwa na polisi kwa tuhuma za kuliendesha
gari lililowabeba wavamizi kuelekea Mpeketoni Lamu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MTU ANAYEMILIKI AKAUNTI YA TWITTER YA AL SHABAAB AKAMATWA NCHINI KENYA.”
Post a Comment