Wednesday, October 8, 2014
RAIS KENYATTA ATUA KWENYE MAHAKAMA YA ICC.
Do you like this story?
![]() |
| Rais Kenyatta wakati akiwasili katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC) huko The Hague. |
![]() |
| Rais Kenyatta wakati akielekea The Hague jana. |
RAIS
wa Kenya, Uhuru Kenyatta, leo yupo mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu
(ICC) huko The Hague, ambako anakabiliwa na mashtaka ya uhalifu dhidi ya
binaadamu.,
Rais Kenyatta ni
kiongozi wa kwanza wa taifa kuwasili mbele ya mahakama hiyo.
Kenyatta amefika
mbele ya mahakama hiyo baada ya waendesha mashtaka kuishutumu serikali ya Kenya
kukataa kuwasilisha ushahidi muhimu.
Kenyatta amekanusha
madai ya kupanga na kufadhili ghasia za kikabila nchini Kenya baada ya uchaguzi
uliokumbwa na utata mwaka 2007/2008.
Kikao cha leo
kitatathmini ombi la upande wa mashitaka la kutaka kuahirishwa kwa kesi hiyo
hadi pale serikali ya Kenya itakapoikabidhi mahakama hiyo ushahidi unaohitajika
kuhusiana na mali ya Rais Kenyatta.
Upande wa utetezi nao
unataka kesi hiyo ifutiliwe mbali ukisema kuwa upande wa mashitaka hauna
ushahidi wa kutosha kwa kesi hiyo kuendelea.
Kiongozi wa
mashitaka, Fatou Bensouda, amewasili mahakamani akisema kesi hiyo iko katika
awamu muhimu sana.
Kenyatta ameamua
kukaa kimya akimtaka wakili wake kuongea kwa niaba yake.
CHANZO:
BBC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
.gif)



0 Responses to “RAIS KENYATTA ATUA KWENYE MAHAKAMA YA ICC.”
Post a Comment