Wednesday, June 4, 2014

POLISI NA MASHEIKH WAVUTANA KUHUSU PICHA YA MAREHEMU NASRA KUWEKWA KWENYE JENEZA



Mvutano mkali umezuka kwenye shughuri ya kuaga mwili wa Marehemu Nasra Mvungi kati ya Polisi,maafisi Ustawi na Masheikh  kuhusu picha ya marehemu Nasra kuwekwa kwenye Jeneza wakati wa kuaga mwili wake kwenye Uwanja wa Jamhuri Jana.

Maafasi wa kike wa Polisi wa Dawati la Jinsia na maafisi wa Ustawi wa Jamii mkoa walikuza Picha ya Marehemu Nasra kwa lengo la kuiweka kwenye Jeneza jambo lililopingwa vikali na viongozi wa dini ya Kiislam wakida jambo hilo ni kinyume na sheria za dini yao.

Hata hivyo baada ya mvuta huo uliodumu kwa dakika 15 ulifikia muafaka baada ya Polisi na maafisi Ustawi kupokea busara za mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini Bw Fikiri Juma aliyeingilia kati mvutano huo walikubali kutoiweka Picha hiyo ya marehmu kwenye Jeneza,

Mmoja wa mapolisi hao aliamu kuichukua kwa uchungu picha hiyo na kuiweka kwenye mkoba wake huku akiseme” Kama wamekataa basi tutaenda kuiweka kwenye Ofisi zetu kama kumbukumbu ya mtoto wetu Nasra”alisema kwa Uchungu Afande huyo.

Akizungumza kwenye hafra hiyo Kaimu Sheikh mkuu wa Mkoa wa Morogoro Sheikh Ally Omar alisema Ingawa tukio hilo la kumuaga Nasra limefanyika Kiserikali haimaanishi kuvunja sheria za dini kwa kuweka picha ya marehemu kwenye Jeneza

“ Mbali ha kuzia Picha hiyo kuwekwa Kwenye Jeneza laki pia Kisheria sisi hatuna mambo ya kuga tukivunja sheria za dini nini nitaulizwa na wakubwa zangu,hivyo kwa sasa sote tusimane na tutaga mwili wa Nasra kwa kusoma dua na baada ya hapo tutaelekea msikiti kuuswalia mwili wa marehemu na baadae kwenda kuuzika.

Marehemu Nasra ambaye alifichwa kwenye Boksi kwa zaidi ya miaka 3 na mama yake Mkubwa Bi Mariam Said alifichuliwa na wasamalia wema May 25 mwaka huu na kutibiwa katika hospital ya mkoa wa Morogoro kabla ya kuhamishi hospital ya Tifa Muhimbili ambako Jumapili iliyopita alifariki dunia na kuzikwa jana makabuli ya mkoa mkoani hapa.

0 Responses to “POLISI NA MASHEIKH WAVUTANA KUHUSU PICHA YA MAREHEMU NASRA KUWEKWA KWENYE JENEZA ”

Post a Comment

More to Read