Wednesday, June 4, 2014

VITENDO VYA UKEKETAJI NA MIGOGORO YA NDOA VYAPUNGUA WILAYANI MAKETE.



Imeelezwa kuwa Matatizo ya ukeketaji na migogoro ya ndoa yamepungua wilayani Makete kutokana elimu iliyotolewa kwa wananchi na shirika lisilo la kiserikali la MASUPHA wakishirikiana na The Foundation for Civil Societies katika kata tano za wilaya hiyo

Akizungumizia kuhusu hilo mkurugenzi wa MASUPHA Bi Aida Chengula amesema mradi huo uliokuwa unadhaminiwa na shirika la  The Foundation For Civil Societies  ambao umetekelezwa katika kata tano ambazo ni  Ukwama, Mang’oto,Kipagalo,Ikuwo,na Mfumbi zote za wilayani Makete

Pia amesema mradi huo ulianza Decemba 27 mwaka 2013 “mradi wetu tumeutekeleza katikakata tano ambapo kila kata tulimujengea uwezo kijana mmoja kwaajili ya kutoa elimu kwa jamii inayo mzunguka kuhusiana na mambo sera ya taifa ya Ukimwi,unyanyasaji wa kijinsia,na elimu kuhusu unyanyasaji wa kijinsia hususan ukeketaji kwa wanawake”

Bi Chengula alielezea faida walizo zipata katika mradi huo kuwa malengo yao yametimia kwani idadi kubwa ya  mambo waliyolenga yametekelezeka ikiwemo kupunguza idadi ya kesi za migogoro ya kifamilia katika mabaraza ya usuluhishi katika kata tano ambazo mradi ulikuwa unatekelezwa na kuongeza kuwa jamii ilikuwa haina elimu kuhusina na mambo ya ndoa ambayo mpaka  kiasi Fulani imepungua kutoka kesi 5 hadi 8 kwa mwezi na kufikia kesi 1 hadi 2 kwa mwezi

Hata hivyo Bi Chengula ameiambia blog hii kuwa licha ya mradi huo kuwa na mafanikio amezitaja changamoto za mradi huo kuwa ni pamoja na watu kuwa na uelewa mdogo wakati wa warsha mbalimbali kwani  wamekuwa wakitaka kulipwa fedha nyingi

“Makete kuna mashirika mengi yanayotoa elimu hivyo watu wamekuwa wakilinganisha viwango vya posho kutoka katika mashirika mengine  hivyo kufanya  mwitikio wa jamii kuwa mdogo”alisema Bi Chengula na kuongeza kuwa  pia kumekuwa na changamoto ya  pesa za mradi kutokufika kwa wakati.

Kwa upande wao vijana waliokuwa wakitoa elimu katika vijiji vya kata zao walieleza kufurahishwa na mradi huo kwani licha ya kusaidia elimu  kwa jamii pia wao wamejengewa uwezo  ambao utawasaidia kujijengea familia bora
“mradi huu umewasaidia wanajamii kubadilika kwa kiasi kikubwa hapa katika kata yetu kumekuwa na tatizo  la akina mama wenye umri mkubwa kujihusisha na mapenzi na vijana wadogo jambo ambalo limekemewa na elimu imetolewa na kumekuwa na mabadiliko kwa jamii hiyo”alisema Neema Sanga muwezeshaji kutoka katika kata ya Ukwama

Naye Frojensia  Sage mwezashaji kutoka katika kata ya  Nkondo alisema kama kijana ametoa elimu katika kata hiyo  na kumesadia kubadilika husasani suala ukeketaji kwa wanawake ambapo mpaka sasa jamii hiyo imeweza kubadilika pia aliongeza kuwa kumekuwa na changamoto za  za utekelezaji ikiwemo vitendea kazi  kama vipeperushi ambavyo vinaweza kusaidia jamii pia kujijengea  utaratibu wa kupata elimu kupitia maandishi kwani yanahifadhika kwa muda mrefu

Bw. Sage alisema pia viongozi wa maeneo husika wamekuwa hawatoi ushirikiano kwa wawezeshaji hao hao

Na Riziki Manfred

0 Responses to “VITENDO VYA UKEKETAJI NA MIGOGORO YA NDOA VYAPUNGUA WILAYANI MAKETE.”

Post a Comment

More to Read