Tuesday, June 3, 2014

SERIKALI IMEKIRI KASI YA KUPAMBANA NA VITENDO VYA UDHALILISHAJI KWA WANAWAKE KWENYE KUMBI ZA STAREHE NI NDOGO.



Serikali imekiri kuwa kasi ya kupambana na vitendo vya udhalilishaji wanavyofanyiwa wanawake kwenye baadhi ya kumbi za starehe hapa nchini ni ndogo

Kauli hiyo imetolewa bungeni Dodoma hii leo na naibu waziri wa habari, vijana utamaduni na michezo Mh Juma Nkamia wakati wa kipindi cha maswali na majibu

Mh. Nkamia amesema kumekuwepo na vitendo vya udhalilishaji na aibu wanavyofanyiwa wanawake katika kumbi hizo ikiwemo kucheza nusu utupu ama wakati mwingine kucheza utupu na vitendo vingine ambavyo ni kinyume na sheria na taratibu za nchi

Amesema tayari hatua zimekwishachukuliwa na serikali ikiwemo kuyafungia mashindano ya miss utalii, na vikundi vya "kanga moko" ambavyo vimebainika kuongoza kwa udhalilishaji na kusema kuwa serikali haitaishia hapo bado itazidi kuchukua hatua kwa vikundi vitakavyokiuka ingawa amekiri kuwa serikali inafanya hivyo polepole

"Serikali makini ni ile inayofanya kazi zake taratibu na kwa umakini, wanasema harakaharaka haina baraka" amesema Nkamia

Vitendo hivi vimeonekana kushamiri kwa baadhi ya kumbi za starehe ambapo wanawake hao hufanya hivyo kwa madai ya kuahidiwa donge nono na wengine wamekuwa wakidhulumiwa mara baada ya kufanyiwa vitendo hivyo vya aibu

0 Responses to “SERIKALI IMEKIRI KASI YA KUPAMBANA NA VITENDO VYA UDHALILISHAJI KWA WANAWAKE KWENYE KUMBI ZA STAREHE NI NDOGO.”

Post a Comment

More to Read