Tuesday, June 3, 2014
WAHINDI 14 WAMEKAMATWA DAR, WAMEINGIA KUFANYA BIASHARA HARAMU
Do you like this story?
Askari wa uhamiaji wamewakamata
watu 14 katika maeneo ya Msasani jijini Dar es Salaam kutoka nchini India na
Nepal ambao ni wahanga wa biashara haramu ya usafirishaji wa binadamu ambapo
watu hao wameingia nchini kinyume na taratibu za uhamiaji.
Kati ya watuhumiwa 14
watuhumiwa 12 ni wasichana ambao waliletwa nchini kwa lengo la kufanya
maonyesho ya nyimbo za asili lakini wakajikuta wakingizwa katika biashara
zingine ikiwemo kucheza muziki katika nyumba za burudani.
Kwa upande mtu
anayedaiwa kuwaleta wasichana hao amesema amewaleta kwa lengo la kufanya
maonyesho ya muziki huku akipinga kuwa wasichana hao hawatumii kinyume na
hivyo.
Naye mwenyekiti wa
serikali ya mtaa wa mikoroshini msasani amewataka wakazi wa eneo hilo
kujiepusha na tabia ya kukaa na wageni bila ya kutoa taarifa mamlaka husika.
Akithibitisha tukio
hilo mkaguzi wa uhamiaji Bw Dotto Romana amesema wanawashikilia watu hao na
watachukua hatua kulingana na mahitaji ya sheria.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAHINDI 14 WAMEKAMATWA DAR, WAMEINGIA KUFANYA BIASHARA HARAMU ”
Post a Comment