Tuesday, June 3, 2014
WATUMISHI 11 WA SERIKALI MBARONI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA.
Do you like this story?
WATUMISHI 11 wa vitengo vinavyodhibiti
dawa za kulevya, wamekamatwa au kuhusishwa na biashara ya dawa za kulevya
katika maeneo mbalimbali nchini.
Hayo yamesemwa bungeni mjini Dodoma na
Naibu Waziri katika Ofisi ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati akijibu swali
la Mbunge wa Kigamboni, Dk Faustine Ndugulile (CCM).
Majaliwa alisema watumishi hao
waliokamatwa na kuhusishwa na dawa hizo, walikamatwa katika kipindi cha mwaka
2012 hadi mwaka 2013.
Alisema watumishi hao walisimamishwa
kazi na kisha kushitakiwa mahakamani, ambapo baada ya kesi zao kusikilizwa,
wapo waliofungwa magerezani na kufukuzwa kazi.
Baadhi ya watumishi hao, kesi zao bado
zinaendelea mahakamani. Majaliwa alieleza kuwa mikakati inayochukuliwa na
Serikali ili kukomesha biashara ya dawa za kulevya ni pamoja na:
Kuundwa kwa Kikosi Kazi cha Kupambana
na Biashara ya Dawa za Kulevya mwaka 2006, Kuendelea kutoa elimu kwa umma,
hususan vijana kuhusu athari zitokanazo na dawa za kulevya na Kutoa huduma ya
tiba kwa watumiaji wa dawa za kulevya aina ya heroin, hasa kwa wanaojidunga.
Mikakati mingine ni Kuongeza uangalizi
wa karibu katika maeneo ya mipaka, yanayotumiwa kuingiza dawa za kulevya, kama
vile viwanja vya ndege, bandari na mipaka ya nchi kavu;
Kutunga sheria mpya ya kupambana na
kuzuia biashara ya dawa za kulevya, itakayoanzisha chombo kipya chenye mamlaka
ya kukamata, kuchunguza na kupeleleza masuala yanayohusiana na udhibiti wa dawa
za kulevya nchini.
Majaliwa amesema pamoja na mikakati
iliyopo na jitihada zinazofanyika, changamoto za kupambana na biashara hiyo ni
nyingi.
Aliwaomba wananchi kutoa ushirikiano
katika mapambano haya kwa kufichua wahalifu na kuwapeleka waathirika wa dawa za
kulevya katika vituo vya ushauri nasaha na matibabu, kupata huduma.
Katika swali lake, Ndugulile alitaka
kujua watumishi wa vitengo vinavyodhibiti dawa za kulevya, wamekamatwa au
kuhusishwa na dawa za kulevya, hatua zilizochukuliwa dhidi yao na mikakati ya
Serikali kukomesha biashara hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WATUMISHI 11 WA SERIKALI MBARONI KWA TUHUMA ZA KUHUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA.”
Post a Comment