Thursday, July 24, 2014
AZAM FC YAGONGA MWAMBA KUKIPIGA NA MBEYA CITY FC, SASA YAITAKA SIMBA SC YA LOGARUSIC.
Do you like this story?
MABINGWA wa ligi kuu soka Tanzaania
bara, Azam fc wamegonga mwamba kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya wagonga
nyundo wa Mbeya, Mbeya City ikiwa ni sehemu ya kujiandaa na msimu mpya wa ligi
kuu unaotarajia kuanza kushika kasi Saptemba 20 mwaka huu.
Afisa habari wa klabu hiyo, Jafar Idd
Maganga alisema wamewasiliana na kocha mkuu wa Mbeya City fc, Juma Mwambusi
kuomba kucheza mechi ya kirafi mkoani Mbeya au Chamazi, lakini imeshindikana
kwasababu wao wameamua kupumzika.
“Tumewasiliana na Mwalimu Mwambusi kuomba
kucheza nao mechi ya kirafiki, lakini imeshindikana kwasababu ametueleza kuwa
baada ya ligi kusogezwa mbele wameamua kupumzika. Kwahiyo hawaendelei na
mazoezi”. Alisema Jafar.
“Tunacheza mechi za kirafiki kwa lengo
la kocha mkuu Joseph Marius Omog kutazama kama wachezaji wake wanaelewa
mafundisho yake”.
Azam ambao leo hii asubuhi walishinda
bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting katika mchezo wa kirafiki uliopigwa uwanja wa
Chamazi wamedhamiria kuomba mechi ya kirafiki na wekundu wa Msimbazi Simba.
Jafar alisema tayari wameshaongea na
makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange` Kaburu` na amewaambia atatoa jibu
siku chache zijazo.
“Kama kuna uwezekano tunataka kucheza
na Simba, Tumeshaongea na Kaburu na kutueleza kuwa atatujibu. Kama watakuwa
tayari, sisi tuko tayari muda wowote kucheza nao”. Alisema Jafar.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “AZAM FC YAGONGA MWAMBA KUKIPIGA NA MBEYA CITY FC, SASA YAITAKA SIMBA SC YA LOGARUSIC.”
Post a Comment