Thursday, July 24, 2014
`BIG BOSI` WA DAR ABARIKI UJIO WA MAGWIJI WA REAL MADRID, AAHIDI KUTOA USHIRIKIANO MKUBWA.
Do you like this story?
Kutoka kulia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidy Meckysadick, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi, Farough Baghozah na Wajumbe, Evarist Hagila na Saad Kawemba |
MAANDALIZI ya ziara ya magwiji wa Real
Madrid ‘Real Madrid Legends’ yamezidi kushika kasi ambapo leo kamati ya
maandalizi imemtembelea mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Saidy Mecky Sadick,
ofsini kwake, Ilala Jijini Dar kwa lengo la kumueleza rasmi tukio hilo la
kihistoria litakalofanyika mwezi ujao.
Kamati hiyo ikiongozwa na mwenyekiti
wake, Farough Baghozah ilikutana na mkuu huyo wa mkoa ambaye alifurahiswa na
jambo hilo litaloweza kufungua fursa mbalimbali ikiwemo kuutangaza utalii wa
Tanzania anga za kimatifa.
Menenja wa ziara hiyo, Dennis Ssebo
amesema kwamba walikaribishwa kwa heshima na mkuu wa mkoa na kuahidi kuwapa
ushirikiano mkubwa, huku akiwa mwenyeji wa magwiji hao wanaokuja kwa mara ya
kwanza barani Afrika.
“Tumepokelewa vizuri na mkuu wa mkoa.
Umetukaribisha kwa heshima zote na ameahidi kutupa ushirikiano mkubwa,” Alisema
Ssebo.
Magwiji hao watatua nchini Agosti 22
mwaka huu na kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya kikosi maalum cha nyota wa
Tanzania Agosti 23 uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam.
Ssebo alisema mechi hiyo itatazamwa kwa
kiingilio cha chini kabisa cha shilingi elfu tano na wanaamini watanzania wengi
wataweza kumudu kwasababu wamepewa taarifa mwezi mmoja kabla.
Miongoni mwa wachezaji hao waliopata
kutamba katika michuano ya La Liga, UEFA na kombe la dunia ambao watatua nchini
ni pamoja na Luis Madeila Figo, Zidedine Zidane, Fabio Cannavaro, Roberto
Carlos , Ronaldo de Lima, Michael Owen na wengineo.
Baada ya mechi ya kirafiki, magwiji hao
watatembelea vivutio mbalimbali vya utalii hapa nchini na kupanda Mlima
Kilimanjaro, jambo ambalo litaonwa na watu wengi zaidi duniani kwasababu hata
Real Madrid TV itakuwepo kurekodi tukio zima.
Ujio wa magwiji hao ni mwaliko wa
kampuni ya Tanzania Sisi ni Nyumbani (TSN), chini ya Mkurugenzi wake, Farough
Baghozah.
Vodacom Tanzania ni miongoni mwa
makampuni yaliyojitokeza kudhamini ziara hiyo. Makampuni mengine ni Fastjet,
Tropical, Pembe Flower, Lake Gas, EFM Radio na Ladger Plaza Bahari Beach.
Hata hivyo nafasi ya kudhamini bado
ipo, waratibu wa ziara hiyo wanatoa wito kwa makampuni na taasisi mbalimbali
kujitokeza kudhamini kwasababu ni fursa kubwa ya kujitangaza kitaifa na
kimataifa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “`BIG BOSI` WA DAR ABARIKI UJIO WA MAGWIJI WA REAL MADRID, AAHIDI KUTOA USHIRIKIANO MKUBWA.”
Post a Comment