Sunday, July 20, 2014
KOZI YA UKOCHA LESENI A SASA KUFANYIKA AGOSTI.
Do you like this story?
KOZI ya ukocha wa mpira wa miguu ya
leseni A inayotambuliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyokuwa
ianze kesho (Julai 21 mwaka huu) jijini Dar es Salaam sasa itafanyika mwezi
ujao.
Marekebisho hayo yamefanyika kutokana
na maelekezo ya CAF ambayo ndiyo itakayosimamia na kuendesha kozi hiyo
itakayoshirikisha makocha wenye leseni B za shirikisho hilo.
Tarehe rasmi ya kuanza kozi hiyo
itatangazwa wiki ijayo. Mwezi uliopita Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
(TFF) kwa kushirikiana na CAF liliendehsa kozi ya leseni B iliyoshirikisha
makocha 29 kutoka Tanzania Bara na Zanzibar.
BONIFACE WAMBURA
OFISA HABARI NA
MAWASILIANO
SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA (TFF
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “KOZI YA UKOCHA LESENI A SASA KUFANYIKA AGOSTI.”
Post a Comment