Wednesday, July 23, 2014
MANISPAA ZA JIJINI DAR-ES-SALAAM ZAJIIMARISHA KATIKA UKUSANYAJI WA KODI ZA MAJENGO.
Do you like this story?
Waziri wa fedha, mhe. Saada Mkuya |
Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Manispaa ya Kinondoni Mwandisi Mussa Natty alisema kuwa Halmashauri yake ina
wenyeviti wa mitaa wapatao 171na watendaji wa kata 34 ambao wanashiriki katika
kufanya kazi ya kuainisha na kuorodhesha majengo kwa uthamini.
“Tumeweza kuyafanyia uthamini
majengo 6,243 yenye thamani ya shilingi 1,493,360 na kodi inayotakiwa
kukusanywa ni shilingi 2,538,712”. Alisema Mhandisi Natty.
Mhandisi. Natty ameongeza kuwa
katika Manispaa yao wamefanya manunuzi ya vifaa vya ofisini ikiwemo magari kumi
ili kurahisisha ufuatiliaji wa mapato pia Halmashauri ya Kinondoni
imefanikiwa kuanzisha mfumo wa malipo ya kielektroniki wa Maximalipo ambao
umerahisisha malipo ya kodi katika maeneo ya karibu zaidi,kuondoa na kupunguza
msongamano wakati wa malipo,kupata kumbukumbu za mlipa kodi kwa urahisi
zaidi,uwazi na urahisi wa kufuatilia mapungufu.
Kwa upande wa Halmashauri ya
Manispaa ya Temeke, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyoBw. Photidas Kagimbo alisema
kuwa wao wametoa mafunzo kuhusiana na uthamini kwa mkupuo kwa maafisa watendaji
wa kata 30 na wenyeviti, pamoja na watendaji wa mitaa 180 wa Manispaa hiyo.
“Tumebaini jumla ya majengo 3,860
yenye thamani ya shilingi 145,652,498 na kiasi cha kodi ni shilingi 218,478.
Alisema Bw. Kagimbo.
Aidha,Bw. Kagimbo amefafanua kuwa
wamefanikiwa kuwapa watumishi uelewa wa matumizi ya TEHAMA katika utozaji wa
kodi za majengo pia halmashauri imeagiza GPS Camera 5 zitakazozosaidia
kuainisha ramani za majengo katika wilaya ya Temeke.
Kwa Halmashauri ya Ilala,
Mkurugenzi wa Halmashauri hiyoBw. Stima Kabikile naye alisema kuwa Kitengo cha
uthamini cha Halmashauri yake kwa kushirikiana na viongozi wa kata na mitaa
wameweza kubaini majengo 6,820 yenye thamani ya shilingi 989,640 na tozo ya
shilingi 1,484,460.
“Pesa hizi zitokanazo na kodi za
majengo zimesaidia kwa kiasi kikubwa katika suala la maendeleo ya halmashauri
za jiji la Dar es Salaam kwasababu zinakusanywa na halmashauri husika”. Alisema
Bw. Kabikile.
Bw. Kabikile ameongeza kwa
kufafanua kuwa, baadhi ya matumizi ya pesa hiyo katika maendeleo ya manispaa
yakeyametumika katikaununuzi wa magari,utengaji wa ofisi na samani zake
zote,ununuzi wa vitendea kazi zikiwemo kompyuta, mashine ya kudurufu na vifaa
vingine vya ofisi.
Halmashauri zimeweza kujitegemea
kikamilifu katika ununuzi na utekelezaji wa majukumu mbalimbali ya kiserikali.
Ushirikishwaji wa wenyeviti wa
mitaa na kata umepelekea majengo mengi kuainishwa kirahisi lakini bado kuna
changamoto zinazozikabili Halmashauri hizi kama ukosefu wa vifaa vya kisasa na
muhimu,kusambaa kwa majengo na mpangilio mbovu wa majengo.
Wananchi wanahimizwa kuona
umuhimu wa kulipa kodi ili kukuza maendeleo ya wilaya zao na pia wanaaswa
kuepuka kufichana majina ya wamiliki halali wa majengo pindi wathamini
wanapofika katika majengo yao kwasababu moja ya changamoto kubwa ambayo
wathamini wamekuwa wakikukbana nayo ni hiyo ambayo inawawia vigumu wathamini
kufanya kazi yao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MANISPAA ZA JIJINI DAR-ES-SALAAM ZAJIIMARISHA KATIKA UKUSANYAJI WA KODI ZA MAJENGO.”
Post a Comment