Wednesday, July 23, 2014
HAWZAT IMAM SWADIQ KUONGOZA MAANDAMANO YA KULAANI MAUAJI YA HUKO GAZA.
Do you like this story?
TAASISI ya Hawzat Imam Swadiq wameandaa maandamano ya kulaani
mashambulizi yanayofanywa na Vikosi vya Israel dhidi ya wananchi wa Palestina
wasio na hatia.
Kwa mujibu wa Msemaji wa Taasisi hiyo Profesa Abdul Shariff, maandamano
hayo yanalenga kuueleza ulimwengu kuwa wananchi wa Tanzania wanalaani mauaji
yanayoendelea huko Gaza Palestina.
Amesema kuwa maandamano hayo ambayo yatafanyika siku ya
Ijumaa Julai 25 mwaka huu yanatarajia kuanzia Kituo cha Daladala cha Boma
na kuishia Kigogo uwanja wa Bibo.
Profesa Shariff ameongeza kuwa wameamua kupaza sauti zao kulaani baada ya
kuona Jumuiya mbalimbali za Kimataifa ikiwa imenyamaza huku mamia ya watu
wakizi kupoteza maisha yao.
Amesema kuwa inasikitisha kuona hata vyombo vya habari hasa vya Magharibi
havitoi nafasi kubwa kwa mauaji hayo ukilinganisha na mauaji yaliyotokea kwa
kulipuliwa kwa ndege Malyasia.
Naye Mwenyekiti wa Taasisi hiyo Sheikh Hamed Jalala amesema kuwa
wamealika viongozi na Mabalozi wa Nchi mbalimbali ili nao waweze kushiriki
katika kupaza sauti zao pamoja na watanzania kulaani vitendo
vinavyofanywa na Israel vya kuua watu wasio na hatia.
Sheikh Jalala amesema kuwa kunyamazia tatizo hilo ni kufanya kosa kwani
hakuna hata dini moja inaruhusu mauaji ya binadamu mwingine.
Amesema kuwa maandamano hayo yatahusisha watu wa dini zote na yamepata Kibali cha Mamlaka husika.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “HAWZAT IMAM SWADIQ KUONGOZA MAANDAMANO YA KULAANI MAUAJI YA HUKO GAZA.”
Post a Comment