Wednesday, July 23, 2014
WAJAWAZITO WALALA MZUNGU WA NNE KITUO CHA AFYA KAMBARAGE -SHINYANGA.
Do you like this story?
Vitanda vya wagonjwa vikiwa vimefungwa kwenye mabox kutokana na kukosekana sehemu pa kuviweka kutokana na ufinyu wa wodi pamoja na upungufu. |
Wakinamama wajawazito na waliojifungua
wakiwa katika wodi moja kwenye kituo cha afya cha Kambarage manispaa ya
Shinyanga kutokana na upungufu wa wodi,hali ambayo inaweza kuhatarisha afya zao
kwa kuambukizana magonjwa.
Daktari anayesimamia kituo hicho Costantine
Hubby alisema
hali hiyo imesababisha wanawake
wajawazito na waliojifungua kulala wawili wawili kitanda kimoja na wengine
kulazimika kuweka magodoro sakafuni huku akitaja changamoto nyingine ni kituo
kukosa chumba cha upasuaji wa dharura kwa wajawazito wenye uchungu
pingamizi pamoja na kutokuwa na gari la wagonjwa hivyo kusababisha usumbufu
mkubwa mgonjwa akiwa amezidiwa hasa wakati wa msimu wa masika mvua zinaponyesha
na kuwa katika hatari iwapo atachelewa kufikishwa kwenye huduma.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “WAJAWAZITO WALALA MZUNGU WA NNE KITUO CHA AFYA KAMBARAGE -SHINYANGA.”
Post a Comment