Friday, July 25, 2014
SERIKALI YAPOKEA MABEHEWA 25 YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 4.3 KUTOKA INDIA.
Do you like this story?
Mkurugenzi Mkuu wa TRL, Mhandisi Kipalo Kisamfu (mwenye tai kushoto),akimuelekeza jambo Waziri Mwakyembe. |
Fundi wa Shirika la Reli Tanzania , Ephrahim Joel akikaza nati ya moja ya mabehewa hayo. |
Baadhi ya mabehewa hayo yakiwa yamepangwa katika njia yake bandarini baada ya kushushwa kutoka katika meli. |
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imepokea mabehewa 25 mapya ya kubebea
kokoto yenye thamani ya sh.bilioni 4.316 kwa ajili ya Kampuni ya Reli Tanzania
(TRL) kutoka Kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industriles Limited ya
India.
Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa hafla
ya kupokea mabehewa hayo Dar es Salaam jana, Waziri wa Uchukuzi Dk.Harrison
Mwakyembe alisema mabehewa hayo ni sehemu ya mpango kabambe wa Serikali wa
kufufua Kampuni ya Reli Tanzania chini ya mapngo wa Tekeleza kwa Matokeo
Makubwa sasa (BRN).
Alisema mpango wa BRN kwa Kampuni ya Reli Tanzania
umelenga kuiwezesha kampuni hiyo kiutendaji ili iweze kusafirisha tani milioni
3.0 ifikapo mwaka 2016 kutoka tani 200,000 zilizosafirishwa mwaka 2012 kupitia
Reli ya kati.
“Katika harakati za kufikia malengo haya makubwa,
Serikali kupitia bajeti zake za mwaka 2012/2013 na 2014, ilitenga fedha kwa
ajili ya kugharamia miradi mbalimbali iliyolenga kuboresha vitendea kazi vya
Kampuni ya Reli Tanzania” alisema Mwakyembe.
Alitaja miradi iliyopangwa ni pamoja na kujenga upya
vichwa vya Treni 8, kununua vinchwa vya treni vipya 13, mabehewa mapya 274 ya
kubebea mizigo na mabehewa ya breki.
Mwakyembe alitaja mradi mwingine ni kununua mashine
ya kushindilia kokoto, kununua mabehewa 22 mapya ya abiria na kununua mabehewa
25 mapya ya kubebea kokoto ambayo yamepokelewa jana.
Katika hatua hiyo Mwakyembe ametumia fursa ?hiyo
kuipongeza TRL kwa kupokea mabehewa hayo kwa wakati na kuishukuru Kampuni ya
Hindusthan Engineering and Industries Limited ya India kwa utengenezaji wa
mabehewa hayo kwa muda uliopangwa.
Alisema lengo ni kuiwezesha TRL kufikia malengo ya
kusafirisha mizigo tani 3.0 na kutembeza treni za abiria tano kwa wiki ifikapo
mwaka 2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “SERIKALI YAPOKEA MABEHEWA 25 YENYE THAMANI YA SH.BILIONI 4.3 KUTOKA INDIA.”
Post a Comment