Thursday, July 24, 2014
TAMBO ZA MTIBWA SUGAR TIMU PINZANI ZINAWEZA KUKIMBIA LIGI KUU.
Do you like this story?
TIMU nyingi zinazoshiriki ligi kuu soka
Tanzania bara zipo katika maandalizi ya kujiwinda na msimu mpya utakaoanza
kushika kasi septemba 20 mwaka huu.
Wakata miwa wa mashamba wa Manungu,
Turiani mkoani Morogoro, Mtibwa Sugar wapo jijini Dar es salaam kujifua katika
fukwe za Koko ili kujiimarisha zaidi.
Mtibwa Sugar chini ya kocha mkuu,
Mtanzania Mecky Mexime, msimu uliopita ilimaliza katika nafasi ya 7 kwa
kujikusanyia pointi 31 kibindoni.
Mabingwa hao mara mbili mfululizo wa
Tanzania kwa mwaka 1999 na 2000 walishinda mechi 7, sare 10 na kufungwa mechi
9. Walitikisa nyavu za wapinzani mara 30 na zao kuguswa mara 31.
Tangu itwae ubingwa miaka miwili
mfululizo (1999, 2000), Mtibwa haijawahi kuwa katika ubora wake na kujikuta
ikishika nafasi za kawaida katika msimamo.
Msimu uliopita walishindwa kutamba
kabisa na kuziacha timu za Azam fc, Yanga, Mbeya City fc, Simba, Kagera Sugar
na Ruvu Shooting kukaa juu yao katika msimamo wa ligi kuu.
Mtibwa ni timu inayoendeshwa kikampuni
na haina matatizo kama klabu za wanachama, lakini haijawa na makali kama Azam
fc na hata pacha wao Kagera Sugar.
Kuelekea msimu ujao, wakata miwa hao wa
Manungu wamesema wanajifua vilivyo ili kurejesha heshima yao iliyopotea kwa
muda mrefu.
Afisa habari wa klabu hiyo, Tobias
Kifaru Lugalambwika amejitapa na kusema kwamba maandalizi yanakwenda vizuri na
wala hakuna haja ya kuifananisha na timu ndogo.
“Mtibwa iko vizuri kweli kweli, moja ya
klabu inayoendeshwa kikampuni, Tunakwenda kwenye mstari, hatuyumbishwi na
watu”. Alisema Kifaru.
Afisa habari huyo aliongeza kuwa Mtibwa
ni klabu bora Tanzania, tofauti na timu changa za Azam na Mbeya City.
“ Hapa Tanzania klabu bora na kongwe ni
tatu tu, Simba, Yanga na Mtibwa”. Alijigamba Kifaru.
“Kuna timu zinawika mwaka mmoja halafu
zinatelemka, halafu unaziona tena baada ya miaka 10 au 15. Mtibwa ipo juu na
usifananishe ni timu nyingine”.
“Maandalizi ni mazuri na msimu ujao
tutafanya vizuri na kurudi katika hadhi yetu. Tunakiri kufanya vibaya kwa miaka
mingi, lakini sasa inatosha”. Alimaliza Kifaru.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “TAMBO ZA MTIBWA SUGAR TIMU PINZANI ZINAWEZA KUKIMBIA LIGI KUU.”
Post a Comment