Thursday, July 24, 2014
MAENDELEO BANK YAANZISHA HUDUMA ZA BIMA.
Do you like this story?
CEO wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba akiongea wakati wa uzinduzi wa Maendeleo Insurance Agency. |
CEO wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba na CEO wa UAP Nick Itunga wakipeana mikono baada ya uzinduzi wa Maendleo Insurance agency |
Wafanyakazi wa Maendeleo Bank na wa UAP wakiwa katika picha ya Pamoja.(Picha na fahari news) |
Maendeleo Bank imezindua
huduma ya bima ikiwa ni lengo la kuwapatia wateja huduma zote muhimu ndani ya
dari moja. Pia inachangia juhudi za serikali kuboresha na kufikisha elimu na
huduma za bima kwa wananchi wengi ambao hawajafikiwa. Maendeleo Bank Insurance
Agency imeanzishwa ili kuunga mkono mkakati
wa Serikali wa huduma za kifedha jumuishi ambazo zitahamasisha wananchi wengi
watumie na wafikiwe na huduma za kifedha ikiwa ni pamoja na bima.
Katika huduma za bima,
Maendeleo Bank Insurance Agency imejipanga kutoa huduma zote za bima isipokuwa
za maisha. Huduma zifuatazo zinapatikana Maendeleo Bank Insurance Agency: Bima
za binafsi na za biashara zikiwemo bima za moto na wizi, bima za magari ya aina
zote pamoja na mitambo, bima za nyumba na vitu vya majumbani, bima za
wafanyakazi, bima za maofisini, bima za biashara, bima za wakandalasi, bima za
vitu vinavyosafirishwa na bima za afya.
Akizungumza wakati
wa uzinduzi wa ‘’Maendeleo Insurance Agency ‘’ Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo
Bank Ndugu Ibrahim Mwangalaba amesema ‘’Kwa kuungana na kampuni ya kimataifa ya
Bima yaani, UAP Insurance ni faida kubwa kwa wateja wa Maendeleo Bank Insurance
Agency kwani UAP Insurance inauwezo mkubwa wa kubeba bima zote zitakazopelekwa
kwao na iwapo itatokea tatizo linalohitaji kugharimia madhara ya kilichowekewa
bima, basi mteja wetu hatasumbuka kwani Maendeleo Bank Insurance Agency
itafuatilia mambo yote kwa muda mfupi iwezekanavyo ili mteja asisumbuke.
Mwangalaba aliongeza ‘’ Bima binafsi au za biashara ni muhimu mno katika
kulinda kipato na mali za wateja wetu, uanzishwaji wa huduma za bima ni kuishi
kwa vitendo katika kauli mbiu yetu ya pamoja nawe katika maendeleo, kwani
tunapenda kuona maendeleo ya wateja wetu yakienda mbele si kurudi nyuma kwa
matukio yanayoweza kuzuilika kwa kuwa na bima’’
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 Responses to “MAENDELEO BANK YAANZISHA HUDUMA ZA BIMA.”
Post a Comment